Nguvu ya Mungu katika kuokoa ndoa zilizopotea

Suala la mahusiano limekuwa likichanganya sana vichwa vya watu wake kwa waume. Utafiti unaonesha kuwa watu hujisikia vizuri pale wanapozungukwa na watu wao wa muhimu na wanaowaamini katika shughuli mbalimbali za kimaisha, vivyo hivyo hata kwenye mahusiano ya kimapenzi ambapo wapenzi wanapoishi karibu huwa na furaha na upendo mkubwa.

Kumekuwa na vita sana siku hizi baina ya wanawake walio katika ndoa na wale wanaoitwa michepuko. Vita hivi vimefanya mpaka familia kuyumba sababu hakuna amani tena. Michepuko wamekuwa wanaonekana vinara na wajanja kwenye vita hivyo pamoja na kwamba sifa yao kubwa ni wezi wa waume za watu.

Dawa ya kukatisha na kuzima vita hivi sasa imepatikana baada ya dada Colle Karyn kufanya semina kwa wanawake walioolewa na wale ambao hawajaolewa wajulikanao kama singles.

Katika kipindi kilichopita Dada Colle Karyn amezungmzia takribani mambo saba katika maisha ya ndoa. Yakiwemo yale ya

  • Suala la kuomba msamaha
  • Kuwa na unyenyekevu katika mapenzi, yaani dhana ya kujishusha katika mapenzi.

Katika muendelezo wa kipindi hiki, leo dada Colle anaendelea pale alipoishia kuhusu mada hii ya leo ya michepuko. Moja ya vitu ambavyo ameendelea kuzungumza ni pamoja na,

SOMA ZAIDI.

Mambo ambayo mke mwema anapaswa kujihusisha nayo

  1. Mke mwema anapaswa kuwa jasiri katika ndoa yake/kutoogopa chochote.

Suala la ujasiri hapa ni ile dhana ya kutoogopa chochote, kama uko na Mungu hauwezi kuogopa chochote hata usikie habari mbaya inatisha kiasi gani. Kitu ambacho mke mwema anapaswa kuwa nacho ni kuhakikisha yuko vizuri na Mungu wake. Mungu atamuonyesha

“Kaa vizuri na Mungu wako wala hautaangahika na mume wako, wala hautaangahika na michepuko, Mungu atakuonyesha kila baya linaloizunguka ndoa yako”-Dada Colle alisema

  1. Mke mwema anapaswa kuhakikisha yuko vizuri na Mungu wake

Colle anasema mke mwema napaswa kukaa vizuri na Mungu wake naye atamuonyesha mabaya yote. Mke mwema anapaswa kuwa jasiri anapoonyeshwa mabaya yote.

“Utaona mwanamke akisikia mume wake ana mchepuko anapanic na atataka amuone mchepuko kama yuko vizuri Zaidi yake”-Colle Karyn

  1. Mke mwema anapaswa kumtegemea Mungu kwa maombi

Mke mwema utegemea maombi. Utegemea msaada kutoka kwa Mungu na sio kuweka mkono kwenye shavu. Mke mwema anapaswa kufanya maombi hata kwa njia ya kufunga. Unapaswa kujiwekea muda wa kufunga kwa ajili ya maombi.

“Amka usiku wa manane omba, achana na maombi ya dakika mbili. Tumia muda mwingi kuomba ili ufanikiwe”-Colle Karyn

  1. Mke mwema asizongwe na Mambo ya Dunia na awe na Amani wakati wote.

Dada Colle anatuambia kuwa mke mwema anapaswa kuwa na Amani na sio kutafakari mabaya juu ya mume wake. Unapaswa kuishi na Amani na sio kuwaza mume wako yuko kwenye mambo mabaya. Vinywa vyenu vijae maneno yanayompa Mungu utukufu bila kujali mazingira.

Katika semina hiyo kumekuwa na mjadala mkubwa na wenye mambo mengi sana ambayo ni makubwa na kushangaza pia kutoka pande zote mbili. DFM ilipata fursa kuhudhuria na kupata mafundisho hayo.

Kwa wewe ambaye haukupa nafasi ya kuhudhuria semina hii na unatamani kujua nini kilichojiri sikiliza D-LOVE hapa hapa. Kwa nondo hizo na shuhuda zake natumaini utapata kitu cha kukubadilisha ama kukutia moyo. Furahia semina hii hapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz