Max Malipo na uchakataji wa miamala ya kielektroniki

Matumizi ya mashine za kuchakata miamala ya kielektroniki nchini Tanzania ni wazi sasa yanazidi kukua siku hadi siku. Licha ya kuwa na changamoto kubwa katika baadhi ya maeneo huduma hii bado inasonga mbele.

Mfumo huu wa ulipaji wa fedha kwa kutumia mashine za kieletroniki umekuja kurahisisha mfumo wa malipo ya bidhaa au huduma. Ambapo awali ilimpasa mteja afike kwenye ofisi inayotoa huduma au kuuza  bidhaa kufanya malipo.

Maxcom Africa ni kampuni ya uchakataji wa miamala kieletroniki nchini Tanzania. kampuni ambayo iliona uwepo wa tatizo la matumizi ya muda mrefu zaidi kupata huduma za kawaida za kijamii (Utility).

Faida sita (6) za kutumia mfumo wa malipo kieletroniki

  • Kupata huduma karibu na nyumbani kwako au mahali popote utakapokuwa
  • Kutunza muda ambao ungeutumia kwa ajili ya kwenda kufanya malipo ya fedha taslimu
  • Kutunza kumbukumbu za manunuzi yako binafsi kwa urahisi
  • Kutunza uwazi katika makusanyo kiujumla
  • Mfumo wa kufanya miamala ya fedha kwa njia ya kieletroniki ni rahisi na salama.

Licha ya kutatua kero mbalimbali zilizokuwa zinawakumba jamii kutoka na kutokuwa na mfumo madhubuti wa kielektroniki. Maxcom pia imekuwa kama chombo kinachoisaidia serikali katika ukusanyaji wa mapato.

Mara mtumiaji wa huduma au bidhaa atakapotumia mashine za Max Malipo kufanya manunuzi basi ni wazi atakuwa amelipa kodi ya huduma au bidhaa anayoinunua moja kwa moja.

Maxcom Africa sasa wanatoa huduma za Malipo ya Kielektroniki katika idara kama vile ya Maji, umeme, Polisi, usafirishaji na katika idara nyingine.

Ni wazi sasa uwepo wa huduma hizi za kuchakata miamala kielektroniki zinatoa ufumbuzi wa tatizo ya upataji mbaya wa huduma. Mtu sasa anaweza kupata huduma popote anapokuwa ilimradi tu awe na kifaa cha kufanya miamala.

Hili kuweza kupata elimu na taarifa mbalimbali za uchambuzi wa kina endelea kutusikiliza kupitia DFM RADIO HAPA au pakua App yetu ya Dfm kwenye Google play store kutusikiliza live.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz