Upekee wako ndo Utofauti wako

Vijana wengi wa leo wamekata tamaa kutokana na yale yanayo wazunguka. Wapo wale ambao wamejikataa na kujiona hawafai mbele ya jamii. Kumekuwa na wale wanaofikia hatua ya kulaumu na kukufuru kwanini alikuepo duniani. Huo ni upande mmoja ambao ni mgumu kwa kijana ambae anapita katika mazingira  magumu.

Tuje upande wa pili sasa kwa wale ambao hawapitii katika hali ngumu, hawa nao kuna changamoto ya kuiga kile au vile mwenzake anaishi. Wengi wamekua na maisha ambayo sio yao na kufikia hatua hata ya kuwa na maisha mawili. Maisha halisi na maisha ya mtandaoni vinakuwa ni vitu viwili tofauti kama maji na mafuta. Wewe kijana unaesoma waraka huu tambua thamani yako na upekee ulionao.

Umewahi kujiuliza kwanini umeumbwa John na si Hamisi au kwanini umeumbwa Asha na si Rose? Kwa swali hilo tu kwanza utajua wewe ni wapekee sasa hatua ya pili ni kujua upekee wako upo wapi. Kutana na Mwalimu Richard Mndalaakitoa semina kwa vijana wote kupitia DFM ndani ya kipindi cha D-YOUTH. Sikiliza kwa kubofya hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz