Tanzania ya Viwanda ni fursa adhimu ya Ajira

Tatizo la uwepo wa ardhi duni isiyo na rutuba ni wazi kunachochea upatikanaji finyu wa malighafi za uzalishaji. Hii ni fursa kwa jamii kutafuta njia mbadala ya kuendelea kuitunza ardhi kwa ajili ya kilimo endelevu chenye manufaa kwa viwanda.

Uwepo wa Sera ya uchumi wa Viwanda nchini ni wazi uzalishaji wa mali ghafi unapaswa kukua kwa kiwango cha hali ya juu sana. Ikizingatiwa sekta ya kilimo ndio chachu ya ukuaji wa viwanda.

Guavay ni kampuni ya Kitanzania iliyoanzishwa na baadhi ya vijana wa kitanzania maalumu kwa ajili ya kutengeneza na kuzalisha mbolea ya asili ya mimea aina ya Organic iitwayo “Hakika Organic Fertlizer”. inayotokana na mabaki ya matunda, mbogamboga na mimea.

Kwanini Guavay waliamua kutengeneza Mbolea ya Asili?

Sababu kuu ya kuamua kuja na mbolea ya asili ni kupotea kwa rutuba kwa ardhi ya Tanzania kulikochangiwa na;

  • Matumizi mabaya ya ardhi
  • Kutotumia mbinu sahihi za kilimo
  • Kutumia Mbolea ambazo zinachosha udongo

Licha ya upatikanaji mgumu wa Malighafi Guavay inapitia hatua kadhaa katika mchakato wa uzalishaji  wa mbolea ya Organic.

  • Ukusanyaji wa takataka zenye uwezo wa kumeng’enywa na wadudu (Bakteria) kutoka kwenye baadhi ya Masoko jijini Dar es salaam.
  • Hutumia mali ghafi kama vile Binder pamoja na mali ghafi zenye kiwango kikubwa cha Nitrogen
  • Pamoja na Brown material ambayo inatumika kuleta mchanganyiko wa uzalishaji wa mbolea.

Guavay sasa inapanga kuondoa kero kubwa ya takataka kwenye majiji yote nchini. Ikiwa kama fursa kwao katika kuongeza uzalishaji wa mbolea ya asili. Huku ikijiwekea malengo ya kuzalisha takribani tani 5000 kwa mwaka ikiwa ni pamoja nakutengeneza ajira zaidi.

Kampuni ya Guavay inaungana na Manispaa ya Kinonondoni katika kuitumia fursa hii ya pembejeo za kilimo. Mara baada ya manispaa hiyo kusaini Mkataba wa zaidi ya sh. bilioni 5.56 na kampuni ya ukandarasi  ya  CRJE ya nchini China. Mkataba huo ni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kiwanda  cha kuchakata taka kuwa mbolea aina ya mboji .

Hili kuweza kupata elimu na taarifa mbalimbali za uchambuzi wa kina endelea kutusikiliza kupitia DFM RADIO HAPA au pakua App yetu ya Dfm kwenye Google play store kutusikiliza live.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz