Uwekezaji na uendashaji wa biashara ya Gesi nchini

Nishati ya gesi asilia imesambaa kote duniani na watu wengi wamekua wakitumia gesi katika shughuli zao za kila siku. Shughuli za majumbani kama vile mapishi na shughuli za viwandani zote hizo zinaweza kutumia nishati ya gesi.

Historia inaonyesha kwa zaidi ya miaka 50, Tanzania imekuwa ikifanya utafiti wa gesi na kwa mara ya kwanza 1974 iligundulika uwepo wa akiba ya gesi asilia kwenye kisiwa cha SongoSongo mkoani Lindi kabla ya kugundulika tena kwenye Ghuba ya Mnazi 1982 huko Mkoani Mtwara.

Deep FM Radio imefanya jitihada za kutafuta wataalam wa gesi ili kutujuza faida na fursa zipatikanazo kwenye gesi. Najua wapo wengi ambao wanatumia gesi lakini hawajui inamchanganyiko gani lakini pia faida zake na fursa. Kutana na Mhandisi Ndaganza Mzonya kutoka PAN African Energy ambae ni mbobevu wa masuala ya gesi asilia.

Nini Maana ya Gesi Asilia?

Gesi asilia ni mchanganyiko wa aina mbalimbali za gesi zinazopatikana ardhini. Ni nishati inayotuwezesha katika matumizi ya shughuli mbalimbali.

Mchakato wa Gesi mpaka kufikia kwenye matumizi

  • ¬†Gesi inatolewa ardhini/baharini katika mfumo Ghafi (Row gas)
  • Inasafirishwa hadi kiwandani (Plant) kwa ajili ya kuchakatwa (Processing)
  • Kuondolewa kwa vimiminika vyote (liquid) ambavyo havihitajiki kama vile maji na vimiminika vingine kama mafuta (hydroCarbon liquid) kwa ajili ya gesi kuwa kavu
  • Kuondoa element zote za maji ambazo haziwezi kuondolewa kwa njia ya kawaida. Huondolewa kwa njia ya kuchanganya na kemikali.

Uwekezaji na ufanayaji biashara ya Gesi nchini.

Shughuli za uwekezaji na ufanyaji wa biashara ya Gesi nchini Tanzania zilianza mwaka 2004 kupitia katika Kisiwa cha SongoSongo na baadae 2006 katika Ghuba ya Mnazi huko Mkoani Mtwara.
Kuanzia mwaka 2010 hadi 2016 sekta ya Gesi nchini ilichukua sura mpya mara baada ya kugundulika kuwa kuna adhina kubwa ya Gesi asilia nchini yenye kufikia hadi futi za Ujazo Milioni 57

Uwepo wa akiba hii ya Gesi unatabiriwa kuwa kuja kuongeza kasi ya uzalishaji wa nishati ya umeme nchini. Lakini pia kuja kuleta mapinduzi makubwa katika sejta ya viwanda pamoja na utunzaji wa nazingira ikiwa ni mkakati wa mtumizi ya gesi majumbani.

Fuatilia kwa umakini kipindi hiki upate kufahamu kuhusu namna gesi inavyopatikana na mchanganyiko wake, faida zake katika maisha ya mwanadamu lakini pia sehem nyeti ambayo wengi wangetamani kusikia ni fursa ya biashara. BOFYA HAPA chini kusikiliza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz