Nini Umuhimu wa Kwaya kwenye makanisa?

Kwa kipindi cha miaka ya nyuma kwaya ndio ilikuwa nembo ya kanisa na umuhimu wa kwaya ulionekana, kwaya ndio iliyokuwa inatambulisha kanisa. Na kanisa lolote lilikuwa likitambuliwa na kwaya husika.

Nini maana ya kwaya?

Kwaya ni kikundi cha watu wanaoimba pamoja na kupiga vyombo vya muziki. Kwaya ni kiungo muhimu katika Kanisa kinachofanya huduma ya uimbaji. Wapo wanakwaya wenye vipaji vya uimbaji, sauti za kuvutia na uwezo wa kutunga nyimbo  mpya.

Zipo kwaya zenye madhui tofauti tofauti lakini hapa tunazungumzia kwaya zenye maudhui ya kusifu, kuabudu na kumtukuza Mungu, ambapo aghalabu uimbwa kwenye makanisa.

Kanisa ni mwili wa Kristo wenye viungo vingi; na kila kiungo kina kazi yake. Kwaya ni moja ya kiungo cha kanisa ambapo kikitimiza vizuri wajibu wake, Kanisa litahudumiwa. (1 Pet 4:10-11)

Kwaya ni muhimu ndio maana hata katika Agano la Kale walikuwepo watu maalum waliowekwa kufanya huduma ya uimbaji (1Nya 6:31-32). Maneno ya nyimbo yana nguvu kubwa. Yanaweza kubadili hali ya huzuni kuwa ya furaha na moyo mgumu kuwa laini. Daudi alipopiga muziki roho mbaya ilimwacha Sauli (1 Sam 16:23)

SOMA ZAIDI:

Kupitia kipindi cha Deep Ibada, kinachorushwa moja kwa moja na Deep Fm, mtumishi wa Mungu Mchungaji Asta Meshack Muhini wa kanisa la T. A. G Mwenge amezungumza kuhusu  misaada kwenye kwaya na umuhimu wa kwaya.

Nini Umuhimu wa Kwaya kanisani?

  1. Kwaya ni Utumishi katika kanisani

Kwaya inafanya kazi ya huduma ya kanisani. Nyimbo zinazopigwa zinashusha uwepo wa Mungu. Zikishusha uwepo wa Mungu madhabahu yanapata nguvu ya mahubiri yake kupitia nguvu zilizoshushwa kutokana na kwaya. Kwahiyo kuanzishwa kwa kwaya kunaleta ustawi wa kanisa.

  1. Kwaya hufanya kazi ya uhudumu.

Miaka ya nyuma, waimbaji walikuwa wainjilisti wenyewe ambao walikuwa wanahubiri kwa njia ya uimbaji. Lakini pia katika kushiriki katika huduma mbalimbali za kikanisa kwenye kanda mbalimbali.

Akizungumza pia na mwendesha kipindi, Mchungaji Asta Meshack Muhini amesema bado anaona matumizi ya kwaya katika kumtumikia Mungu yana tija licha ya uwepo wa waimbaji wengi wa binafsi.

Amesema waimbaji wengi wa binafsi bado wanaangalia kwa ajili ya kupata fedha, hivyo wengi wao hutumia  uimbaji wa nyimbo za injili kama njia ya kujipatia kipato.

“Ibilisi ameingiza roho ya ubinafsi ambayo hailengi katika utumishi hasa lakini inalenga katika kupata fedha, waimbaji binafsi leo hii wakialikwa kwenye mkutano wa Injili watauliza mmeandaa hela kiasi gani?”-Alisema Mchungaji Asta Meshack

Kipindi cha D-IBADA ndani ya DFM kinakuletea mahojiano na Mchungaji Asta Meshack Muhini wa kanisa la T. A. G Mwenge akizungumzia kuhusu  umuhimu wa kwenye makanisa. Sikiliza hapa hapa kwa kubofya hapa chini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz