Msikilize Producer wa Angel Benard wa “Siteketei”

Kwenye kazi za muziki kuna kitu kinaitwa lebo (label), wanamuziki wanajua naongelea nini hapa. Wanamuziki wengi ufanikiwa kutoka kimuziki baada ya kuwa na lebo inayowaangalia katika kazi zao za sanaa.

Suala la kuwa na lebo kwa upande wa nyimbo za injili au muziki wa injili inaonekana ni gumu sana, inawezekana hii ni kwa sababu ya jamii kutotolea macho sana upande huu japo kwa sasa imeonekana kutikisa kwa namna yake..

Godwin Emmanuel maarufu kama OG Kizz yeye ni muaandaji (Producer) wa nyimbo za injili nchini Tanzania. Pia yeye ni mkongwe kwenye kazi hizi za kuandaa muziki. Ameandaa nyimbo kama “Nikumbushe wema wako” wake Angel Benard, “Yote mema” wake Joel Lwaga. Pia amefanya kazi na wasanii kama vile Flora Mbasha pamoja na Bony Mwaitege.

Akiongea moja kwa moja na DFM, Mr. OG Kiz amejaribu kutoa majibu kitaalam na kutoa ushauri wake pia kuhusu kwanini wasanii wengi wa muziki wa Injili wanakosa lebo za kuwaangalia.

“Lebo si kitu rahisi kama tunavyofikiria, lebo ni muonekano wa msanii kwenye kazi zake kwa kila kitu”-Alisema OG

OG ametoa sababu kubwa ya wasanii wengi wa muziki wa injili kutokuwa na lebo zinazowaangalia.

SABABU ZA WASANII WA MUZIKI WA INJILI KUTOKUWA NA LEBO

  • Uwekezaji Mdogo kwenye tasnia

OG anasema asema wao uamini kuwa muziki wa injili ni uimbaji wa madhabahuni hivyo hata malipo yake hutoka madhabahuni

“Bible inasema wa madhabahuni watakula madhabahuni, kwahyo sisi tunahesabu sehemu ya uimbaji ni madhabahu, kwahiyo unabidi upate pesa, wengi hatuwezi kumudu lebo kwa sababu ni gharama, lebo si kitu rahisi”-Alisema OG

  • Hali ngumu ya kiuchumi

OG anasema hali ngumu ya kiuchumi ya baadhi ya waandaji inasbabisha kwa kiasi kikubwa kutokuwa na wasanii wanaoweza kuwaangalia kwa wakati wote.

“Ni ngumu kumudu kuendesha lebo kama haujainvest, kama hauna uchumi mzuri, ni gharama”-Aliendelea OG

Kutokana na kupenya kwa kina zaidi kwa muziki wa injili nchini Tanzania kwa sasa, ni wazi uwekezaji mkubwa unahitajika. Muziki wa injili unakua siku hadi siku huku tukishuhudia wasanii mbalimbali wenye uwezo mkubwa wakijitokeza.

Ni suala la wadau wa tasnia hii kuiangalia kwa macho ili muziki wetu wa injili uzidi kupenya mbali zaidi. Ili tufike  kama vile wa wenzetu, Nigeria na hata Afrika Kusini.

Sikiliza hapa D-HITS ili kupata stori kamili na ufafanuzi kuhusu suala la lebo (label) kwenye muziki wa injili na umuhimu wake kwa waimbaji. BOFYA HAPA chini kwa kusikiliza vipindi vingine vingi vya DFM.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz