“Fedha za kufanya biashara zipo nyingi sana”-Basil Malaki

Baadhi ya watu mbalimbali wamekuwa wakilalamika kupata wakati mgumu katika kufanya biashara zao, wapo wanaoamua kuachana kabisa na biashara zao kutokana na changamoto wanazokumbana nazo katika uendeshaji wa biashara hizo.

Ni wazi uendeshaji wa biashara unahitaji misingi, nguzo na kanuni za kibiashara ili uweze kufikia malengo mahususi katika biashara yako, Basil Malaki yeye ni mtaalamu wa masuala ya biashara na Ujasiriamali ambapo alitumia fursa ya kuongea na Dfm Radio kuelimisha jamii kuhusu njia na misingi bora ya kukuza biashara.

Misingi Bora (4) ya kukuza biashara yako

  • Kwanza kabisa, unapaswa kujenga uhusiano mzuri na timu yako.

Uangalie nani unataka kufanya nae biashara na ana vigezo vipi vya kufanya biashara na wewe, ikiwemo ujuzi, elimu tabia na kadhalika. Tafuta mtu ambaye unaona ana vigezo ambavyo wewe hauna ili kuleta utofauti na ufanisi. (Diversity skill)

 

  • Pili, ulete suluhisho ambalo linatatua changamoto za watu katika jamii.

Biashara yako lazima iwe inatatua changamoto za watu. Unapaswa kuangalia ni nini ambacho kipo kwenye soko na ambacho hakipo kwenye soko na ni nini kinahitaji kuboreshwa.

         “Hauwezi tu kusema kwakuwa Bakhresa anafanya biashara na wewe ukasema uuze juisi,      yeye aliangalia kuna tatizo au changamoto Fulani fulani” –Bwana Malaki 

Hii inaweza kukusaidia katika mzunguko wako mzima wa biashara yako ili biashara yako iweze kukua kwa ufanisi mkubwa. Itakusaidia katika kupata mrejesho wa biashara yako.

  • Unapaswa pia kuwa na mtu au mwalimu anayeweza kukusaidia kukuza biashara yako (Mentor).

Katika kuendesha biashara yako kwa ufanisi unahitaji kuwa na watu unaoweza kufanya nao biashara katika kuongeza ufanisi wa biashara.

Bwana Malaki anasema kuna utofauti mkubwa wa uchangamkiaji na uwasilishaji wa fursa za kibiashara katika nchi za Afrika Mashariki huku Kenya ikionekana kufanya vizuri katika Nyanja hizo.

Katika jitihada za kukuza uchumi nchini, Bwana malaki anasema tatizo kwa sasa si fedha za uwekezaji kwenye biashara bali ufanisi kwa vijana hasa katika kupanga mawazo yao ya kibiashara pamoja na uwasilishaji wake umekuwa changamoto kubwa kwa sasa.

“shida sio upatikanaji wa fedha, shida ni je? ukija kutafuta fedha umejenga msingi ambao utamvutia mtu akaja kuwekeza kwako, mashirika yana hela nyingi sana lakini shida,  je? una suluhisho ambalo linakuja kutatua changamoto, lazima utupe sababu ya kukupa wewe hela”-Bwana Malaki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz