Mchango wa Mahusiano kwenye Sanaa ya Muziki

Mahusiano uchukua nafasi kubwa sana katika maisha ya binadamu. Kwa namna moja ama nyingine suala la Mahusiano linaweza kuwa na matokeo chanya lakini wakati mwingine linaweza kuleta matakeo hasi kutoakana na jinsi wahusika watakavyolichukulia.

Ni jambo la kawaida kwa siku za hivi karibuni kuona kuwa baadhi ya wasanii wa Muziki wa Bongo Flava na hata wale kutoka tasnia nyingine za burudani wakiwa wanatumia mbinu ya mahusiano katika kuwasilisha Sanaa zao, maarufu kama “Kiki” kama vijana wa mjini wanavyosema.

Kupitia kipindi cha D-Love kinachorushwa na Radio ya Mtandaoni (Online Radio) ya DFM, msanii wa kizazi Bongo Flava, Luminaly anasema yeye haamini suala la mahusiano kwenye kazi zake za muziki licha yay eye kuwa kwenye mahusiano kwa Zaidi ya miaka 10.

Luminaly anasema unapokuwa msanii, wasichana wengi watakuwa wanakufuata lakini kwake changamoto hiyo anajitahidi kuikwepa akiamini kuwa kutumia mahusiano kama sehemu ya kick kuzipeleka kazi zake mbele sio njia sahihi ya kuwa na maisha marefu kwenye Sanaa.

kinachokuja haraka kinaondoka haraka, na kinachokuja taratibu kinaishi, ukitumia kiki utakuja kweli, tutakusikia, tutakufahamu lakini mwisho wa siku ni kama Upepo, unapita”-Alisem Luminary

Mchango wa Mahusiano kwenye Sanaa ya Muziki

Wapo wasanii ambao wao uona kuwa suala la mahusiano linaweza kuleta mchango chanya katika kazi zao za Sanaa. Wengi wao ndio ambao utumia mahusiano kama sehemu ya kujitangaza hasa pale wanapokuwa wanakaribia kutoa kazi zao mpya.

Kwa Luminary kwake ni tofauti ambaye licha ya kuwa kwenye mahusiano kwa Zaidi ya miaka kumi tena kwa mtu ambaye ana nafasi ya kufahamika, hajawahi kutumia nafasi ya mahusiano katika kuzitangaza kazi zake za Sanaa.

Suala la kutumia mahusiano kwenye Sanaa (Kiki) limekuwa gumzo sana nchini kutokana na wimbi kubwa la wasanii kuona kama ndio njia pekee inayoweza kufanya kazi zao ziwe juu.

Changamoto wanazozipata wasanii kwenye mahusiano.

Licha ya wimbi kubwa la wasanii kuona kuwa mahusiano yanaweza kutumika katika kuzitangaza kazi zao, lakini pia huwa wanapitia changamoto mbalimbali katika suala zima la mahusiano

 

  1. Muda

Luminary anasema yeye kama yeye anaona mahusiano yanaweza kukufanya ushindwe kutumia muda wako vizuri hasa ule muda ambao ulipaswa kuutumia katika kufanya kazi za Sanaa, na unajikuta kuwa unatumia muda huo kwa ajili ya kutunza mahusiano yako.

 

  1. Wimbi kubwa la wanawake ambao huwatafuta mara kwa mara

Luminary anakiri kuwa suala la umaarufu wakati mwingine linaleta changamoto kubwa kwa jamii. Anasema Iiafikia wakati huwa wanajikuta wanatafutwa na wanawake tofauti tofauti mara kwa mara na kama hawatakuwa makini wanaweza kujikuta wanapoteza malengo ya kazi zao za Sanaa.

 

Si kila mtu anapenda kuweka wazi mahusiano yake, wapo wasanii ambao hutumia mahusiano hasa na wanawake ambao maarufu katika mbinu mojawapo ya kujijenga kikazi Zaidi, lakini wapo ambao wanaona kuwa kutumia njia ya mahusiano ni kama kuharibu kazi na jina ambao amelijenga kwa muda muda Fulani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz