Mapito ya maisha ya Bi Christina Kimani

Ukiwa kama binadamu unaweza kupitia mapito mbalimbali. Unaweza kupitia magumu mengi ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kukurudisha nyuma. Yote haya ni sehemu ya majaribu kama binadamu. Lakini wale waliopitia mapito hayo na bado hawakumuacha Mungu basi walipata kuiona kesho yao.

Kutana na shujaa wa siku Bi. Christina Joseph Kimani maarufu sana kwa jina la mama Kavemba kwenye kipindi cha D-Testify akizungumza moja kwa moja na muendesha kipindi Aaron D.  Ilan.

SIKILIZA ZAIDI

Mwanzo wa safari ya shida na Raha ya Bi christina

Safari ya maisha ya mapito kwa mama Kevemba ilianza miaka ya 70 kama mwenyewe anavyodai. Maisha yake ya vikwazo yalikuwa yanampa simanzi mara kwa mara kabla ya kuamua kumrudia Mungu wake.

Bi. Christina alianza maisha ya kumtumikia Mungu akiwa bado hajaokoka licha ya kukiri kuwa mahubiri ya watumishi wa Mungu mbalimbali yalimpa hamasa na kuamua kuokoka mwaka 1978 katika kanisa la Mwenge.

Sababu kubwa ya yeye kuokoka ni kutokana na ajali ya pikipiki aliyowahi kuipata katika miaka hiyo ya 70. Katika ajali hiyo ya pikipiki,mama Kavemba alikiri kumpoteza mume wake kipenzi kwenye ajali hiyo.

“Tulikuwa kwenye pikipiki mimi na baba watoto wangu, yeye alifariki hapo hapo kwenye ajali. Kwakweli mimi Mungu alinisadia, nikapelekwa Muhimbili kwa matibabu”-Bi Christina alisema

Bi. Christina anasema mara baada ya kupata matibabu kutoka Muhimbili alipata kusikia maneno ya watu mbalimbali ambao walikuwa wanakiri na kushuhudia kuwa Yesu anaponya. Hapa ndipo ilipoanza safari ya mama Kavemba kumpokea Yesu.

Licha ya kuwa Bi. Christina kudharau mara kwa mara maneno ya ushuhuda juu ya Yesu anaponya, anasema lakini hakusita kuyatilia maanani maneno hayo na baadae kuanza kuyafanyia kazi.

Maisha ya Wokovu ya Bi. Christina

Maisha ya wokovu ya Bi Christina anasema ni ya furaha na upendo sana hasa kwa mchungaji wake pamoja na mama mchungaji. Maisha haya aliyafurahia sana licha ya kukiri kubadili kanisa alilokuwa akisali hapo awali.

Katika maisha yake ya wokovu Bi Christina amekuwa akilitumikia kanisa hasa pale alipobarikiwa kupata nafasi ya kuwa karani wa kuhesbau sadaka za kanisa (cashier).

Bi Christina anasema maisha ya wokovu kwa wakati huo yalikuwa ya kujitoa kwa hali ya juu.

Kwa sasa Bi Christina ni mwalimu wa masomo ya neno la Mungu akitoa mafundisho mbalimbali.

Kuwa wa kwanza kusikiliza  kipindi chako bora cha D-Testify kupitia deep fem radio ili uweze kupata shuhuda mbalimbali. Sikiliza kupitia mtandao au kwa kupakua App ya deep fm kwenye simu yako. TUSIKILIZE HAPA. Bofya HAPA chini kusikiliza kipindi hiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz