Mitazamo ya wengi juu ya waimbaji na wasanii wa nyimbo za injili, hasa wenye majina makubwa, ni kwamba wana maisha tofauti sana na raia wa kawaida. Hii ipo sana sio tu kwa waimbaji hata waigizaji na wanamichezo. Kwanza ikumbukwe wao pia ni binadamu kama wewe na wamezaliwa kama wewe ulivyozaliwa.

Kwa kutoa ukakasi uliopo baina ya raia na wasanii, Solomon Mkubwa muimbaji wa nyimbo za injili amekuja kumaliza mzozo huo. Yeye ametetea hoja hiyo kwanza kwa kueleza yeye ni nani lakini pia alizama ndani kidogo kueleza maisha yake tangu anazaliwa mpaka hapo alipo.

Ndugu Solomon aliwahi pata matatizo katika maisha yake na hakusita kueleza nini kilimkumba mpaka kufikia hatua ya kuwa na mkono mmoja wakati alikuwa mzima kama wewe. Sikiliza story hii ya Solomon ndani ya DFM kwenye kipindi cha D-HITS, bofya hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz