Mahusiano Nje ya Utaratibu

Mashine ni kifaa chochote ambacho hutumika kurahisisha kazi. Mfano kisu ni mashine ambayo hutumika kurahisisha kazi ya kukatakata vitu kama vile nyama, nyanya, matunda n.k. lakini kisu hicho hicho kinaweza kutumika kwa matumizi mengine pia kama vile silaha inayoweza kutoa uhai wa binadamu au hata mnyama. Mahusiano nayo ni kama kisu. Yanaweza yakawa mazuri kwa upande mmoja au kuwa mabaya kwa upande mwingine.

Mwalimu Mitimingi Peter Mitimingi anafundisha madhara ya kuwa na mahusiano nje ya utaratibu wa ki-Mungu kupitia DFM.Mwl.

Peter Mitimingi kupitia youtube  anasema utaratibu wa ki-Mungu hauna “boyfriend wala girlfriend” na kwa wanaofanya hivyo basi wameanzisha mahusiano nje ya utaratibu wa Mungu. Utaratibu sahihi ni uchumba halafu hatua ya ndoa ndo ifuate. Zipo hasara mbalimbali anazoweza kupata mtu akiwa kwenye mahusiano yaliyo nje ya utaratibu wa Mungu.

Je, unafahamu njia za kuwa na mahusiano ya utaratibu wa kimungu? Sikiliza kipindi cha D-LOVE kupata nondo nyingi zaidi kuhusu mahusiano na vimbwenga vyake kwa kubofya hapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz