Jinsi ya kufanya biashara ya Magari bila kumiliki Yard

Je, umeshawahi kufikiria kufanya biashara ya Magari?. Je unadhani unahitaji kiasi gani cha fedha? Au unafikiri hauwezi kufanya biashara ya magari bila kumiliki kituo cha kuuzia magari (Yard)

Wapo wafanyabishara wengi wanaojishughulisha na uuzaji wa magari nchini Tanzania na Duniani kiujumla. Lakini ufanyaji wa biashara zao utofautiana kutoka na njia, taratibu na kanuni wanazotumia.

Bwana Lawrence Mwantima ni mshereheshaji na mfanyabiashara wa kuuza magari nchini Tanzania, anamiliki kampuni ya Mwanti Car Trade, uagiza magari yake kutoka nje ya nchi hususani nchi ya Japan. Anafanya shughuli hiyo ya magari bila kumiliki yard. Wateja wake ni wa kuagiza.

SOMA ZAIDI:

Bwana Mwantima upokea oda kutoka kwa mteja na kisha uanza taratibu za kuagiza gari ambayo mteja wake ameiomba nje ya nchi kwa njia ya mtandao kabla ya kumfikishia mteja wake pale alipo. Hapa anatueleza hatua za kufanya biashara ya magari ya kuagiza mtandaoni.

 

Njia 5 (tano) za kuanza biashara ya Magari ya kuagiza mtandaoni.

  • Mapya au yaliyotumika

Kabla haujaanza taratibu zote za kuagiza mgari toka nje u unapaswa kujua magari unayotarajia kuwauzia wateja wako ni yale yaliyotumika au ya mapya. Hii itakusaidia kupata muongozo wa baishara yako.

  • Kufanya uchunguzi wa muundo mzima wa bishara

Unapaswa kujua magari yanapatikana wapi? na pia yanapatikanaje? Wale unaofanya nao biashara pesa inawafikiaje, Napata mzigo wangu muda gani? Na usalama wake ni mkubwa kiasi gani? Ninapata faida gani?

  • Kufanya utafiti wa Ki-bank

Baada ya kufanya utafiti wa biashara yako unapaswa kufanya utafiti pia wa ulipaji na utumaji wa fedha kwa kutumia Bank kutoka nchini kwako. Unapaswa kujiuliza, kununa bidhaa Japani nafanyaje? Nalipiaje bidhaa? Natumaje pesa? Nawezaje kukamilisha malipo?

  • Kuweka Imani.

Kabla haujaanza  kuagiza magari unapaswa kuondoa hofu ya kufanya kazi hiyo kwakuwa kuagiza magari inahusisha kutuma pesa kwa mtu usiyemfahamu lakini pia unafanya biashara na mtu usiyemfahamu.

  • Fanya matangazo ya huduma  yako.

Biashara yeyote inahitaji uwekezaji mkubwa wa kujitangaza. Ni vigumu sana kuuza magari bila kuwa na kituo maalumu pasipo kuwa na kujitangaza. Tumia mitandao mbalimbali kueleza shughuli unayoifanya.

Zipo changamoto kadhaa ambazo unaweza kukutana nazo katika ufanyaji wa baishara hii

 

Changamoto unazoweza kukutana nazo.

  • Hofu

Unaweza kupata hofu kubwa kufanya biashara hii kwakuwa unafanya makubaliano na watu ambao hauwajui, kampuni ambayo hauijui. Hivyo wafanyabiashara wengi hujengwa na hofu.

  • Uwepo wa makampuni makubwa.

Makampuni makubwa uwekezaji wake huwa mkubwa pia, hutumia njia nyingi za kutengeneza masoko ya magari yao, uwekezaji kwa kiasi kikubwa katika magari na matangazo.

Hili kuweza kupata elimu na taarifa mbalimbali za uchambuzi wa kina endelea kutusikiliza kupitia DFM RADIO HAPA au pakua App yetu ya Dfm kwenye Google play store kutusikiliza live.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz