Zitambue sifa za Mtumishi wa Mungu wa kweli

Ni Maisha uliyonayo yanakutakutambulisha kama nani mbele za waliokuzunguka?. Wasifu huo unasadifu majina unayoitwa? Ni wazi kwamba utashtuka hasa kwa wewe ambae unaitwa majina kama vile mbabaishaji, tapeli au muongo. Lakini unaweza usishtuke kama utaitwa Mtumishi wa Mungu.

Majina unayoitwa hata kama ni kwa utani jaribu kuchunguza maisha yako na tabia ulizonazo. Kwa wale ambao wanaitwa watumishi wakati sio watumishi wajaribu kujichunguza pia.

Kupitia kipindi cha D-Ibada cha Dfm radio Mtumishi wa Mungu Nyambele Zephania ambae amekulia maisha ya kanisani akiwa. anajaribu kueleza mfumo ambao ameishi na kupitia hayo basi utapata kujua mengi.

SOMA ZAIDI:

Mtumishi wa MUNGU ni nani?

Mtumishi wa mungu ni yule mtu ambaye kwa hiyari yake mwenyewe amekubali kumpokea Yesu kristo kuwa bwana na mwokozi wake, kujifunza mafundisho sahihi ya neno la Mungu, kuyanyenyekea, kuishi katika yale mafundisho sahihi ya neno la Mungu.

Sifa za msingi za mtumishi wa Mungu.

  1. Uhusiano wake na Mungu.

Jinsi na namna anavyoyachukua mafundisho na neno la Mungu na kuyaishi ndipo anapotengeneza uhusiano mzuri na Mungu. Mtumishi wa Mungu anapswa kufuata misingi ya neno la Mungu ya kuliishi tena kwa unyekekevu.

  1. Mtu ambaye ni mkweli

Mtumishi wa Mungu ni Yule mtu mwenye kulishika neno la Mungu na kulitekeleza. Anapaswa kuwa mkweli, mwenye kusema kweli daima.

Neno la Mungu linakatakaza kusema uongo, daima tunapaswa kusema ukweli. Mtumishi wa Mungu hapaswai kuwa na makona kona.

  1. Muungwana

Uungwana ni sifa kubwa sna. Ni wazi Mtumishi wa Mungu anapswa kuwa muungwana na mnyoofu pamoja na kuaminika mbele za watu.

  1. Mtumishi wa Mungu anapaswa kuwa hofu ya Mungu.

Anapaswa kuwa na hofu ya Mungu kwa ila jambo analolifanya na hata kuliona.

Kuwa na hofu ya Mungu ni kuvitumikia vyote ambavyo vimefundishwa na Mungu ikiwa ni pamoja na kufuata matakwa yake.

“Wapo watu ambao wameingia tu kwenye utumishi wa Mungu sio tu kwa ajili ya kuitwa na Mungu. Bali tu kwa sababu ya mihemuko au marupurupu Fulani. Waliodhani kuwa kanisani kuna manufaa”- Mtumishi Nyambele  Zephania

Kanisa la Mungu ni mfano na familia. Aina ya familia ambayo mtu anatoka ndio inayomtambulisha yeye ni nani. Kama umetoka kwenye familia ya watu wa hovyo hvovyo au wachawi utapata tabu sana kujitambulisha namna nyingine. Kwa sababu watu watakuwa wanakusoma hivvyo hivyo kutokana na familia uliyotoka.

Nakumbuka wale waliokua wakiitwa maprofesa wakati wanasoma shule za secondary? Wale waliokuwa wakiitwa maripota, walimu, wachungaji na wasanii? Je, wewe ulikua unaitwa jina gani? Kuna athari zozote za kukubaliana na majina Fulani ambayo sio halisi? Fuatilia kipindi hiki cha D-IBADA HAPA HAPA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz