Moja ya vitu ambavyo watu wengi wanaangalia kwenye nyimbo za injili ni maudhui ya wimbo huo. Kumekuwa na mijadala tofauti tofauti kuhusu nyimbo za injili na maudhui yake. Ukiacha maudhui hayo kuna mavazi pia ambayo huwa wainjilishaji ama waimbaji wa nyimbo za injili mengine yamekuwa maswali kwa watu, mengine yamekuwa majibu lakini mengine yamekuwa sintofahamu.

DFM katika kutafuta majibu hayo ilikutana na Emmanuel Mgaya ajulikanae kwa jina maarufu la Masanja Mkandamizaji. Masanja alitoa ushirikiano mzuri kujibu maswali aliyoulizwa na pia kueleza namna wimbo wake ulivyopokelewa na jamii. Wimbo wake unajulikana kwa jina la KEMEA PEPO na amesema yeye amefurahi kwa sababu wimbo wake umekuwa tiba.

Je, watamani kujua tiba hiyo ni ya aina gani? Sikiliza D-HITS mwenyewe usisubiri kusimuliwa uhondo huu wa kumsikia Masanja akitema cheche zake kuhusu tasnia hii ya muziki wa injili. Bofya hapa chini kwa kusikiliza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz