Teknolojia imeonekana kuzungumziwa sana na wafanya biashara. Mitandao sasa hivi imekuwa majukwaa ya  kibiashara. Ilikuwa ni kawaida kuona watu wakizunguka huku na kule kunadi, kupiga debe au kufanya mnada wa kuuza bidhaa zake, lakini mambo yamepinduka sikuizi hadi kufikia hatua ya kukaa na maduka au masoko mkononi.

Swali linakuja kwamba wote wanafanya biashara zinazofanana lakini bado wanauza na kupata faida. Pamoja na hayo yote kuna baadhi ambao wameshindwa na kujikuta wanapata hasara. Dr. Said Said  ni mtaalam wa biashara na masoko hasa katika mitandao, akiwa pia ni muasisi wa kampuni ya Online Profit

Kupitia  D-BUSINESS anachambua jinsi ya kutumia mtandao kama jukwaa la biashara. Aidha alibainisha makossa ambayo wengi wanayafanya na kusababisha kushindwa kuendesha biashara zao, lakini pia alikuja na njia mbadala za kuwasaidia wafanya biashara wa aina hiyo. Sikiliza nondo hizi hapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz