Jinsi ya Kupata Mume Mwema

Ukisoma katika biblia  kitabu cha MWANZO 2:18 inasema Bwana Mungu akasema, si vyema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana nae. Wengi wamekuwa wakitafsifiri vile ambavyo wanajua wenyewe na kufanya maamuzi yao. Katika zile harakati za wanawake ama mabinti kutafuta wenzi wao wa maisha wengi hutumia njia za mikato ili kufanikisha kusudi lao.

Nafasi ya wazazi na watumishi katika kuwaelekeza mabinti zao iko wapi? Mabinti wengi wamekuwa wadandiaji wa ndoa za watu na kuanza kuitwa michepuko mda huohuo binti huyo anaeitwa mchepuko wa mtu anatamani kuolewa na anatarajia kuwa mke wa mtu siku moja.

Kama wewe ni binti au mama unaetarajia kuolewa sikiliza semina hii ya mtumishi wa Mungu dada Colle Caryn wa huduma ya Annointed Room kupitia DFM akiongea na wanawake wote akifundisha namna au njia za kupata mme mwema na ndoa inayodumu, ndani ya kipindi cha D-LOVE, hapahapa usitoke wala usizime data.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz