Je? Unajua unaweza kumiliki kiwanda kwa sh. 2500/=?

Ile ndoto ya kumiliki Kiwanda kwa kila Mtanzania ni wazi si dhana ya nadharia tu bali wapo wanaoitumia fursa hiyo. Si tu kwa kuanzisha viwanda kwa wao binafsi bali hata kuwawezesha wengine kuingia kwenye mfumo huu wa uchumi wa Viwanda.

JATU (Jenga Afya Tokomeza Umasikini) ni kampuni ya umma na ya kitanzania ambayo inajishughulisha na masuala ya  kilimo, viwanda na masoko huku lengo kuu likiwa ni kujenga afya na kutokomeza umaskini kwa kutumia rasilimali watu, kilimo na viwanda.

Kampuni ya JATU;

  • Inamiliki mashamba kwa ajili ya kuzalisha mali ghafi kama vile Alizeti, Mahindi na Mpunga.
  • Inazalisha bidha kama vile Nafaka, mafuta na Vinywaj
  • Inamiliki Viwanda kwa ajili ya kuchakata bidhaa zinazotolewa kwenye mashamba yao.
  • Inauza bidhaa zake kutoka kwenye viwanda vyake kwa wanachama wake.
  • Unaweza kununua bidhaa yeyote ya matumizi ya kawaida na kujitengenezea kipato kutokana na gawio la faida za bidhaa za kampuni.
  • Ina wanachama zaidi ya 200 ambao wanamiliki Hisa

Faida za kujiunga na Kampuni ya JATU

  • Kuingiza kipato cha fedha hata ukiwa uko nyumbani kwako kwa kutumia tu bidhaa za JATU
  • Mwanachama kupata nafasi ya kuwa miongoni mwa wamiliki wa viwanda kutokana na kiasi cha Hisa alichowekeza.

Kampuni ya JATU imewekeza kwenye viwanda kwa kiasi kikubwa. Huku ikitoa fursa kwa watanzania ambao wanaotamani kumiliki viwanda kuwekeza kiasi kidogo cha hisa kwenye viwanda vyao, ili kuweza kuwa sehemu ya umiliki wa viwanda.

Hii ni fursa ambayo inatolewa kwa vijana hasa wale ambao wamekosa ajira, wenye ajira na hata wale ambao kwana namna moja ama nyingine wangetamani kuwa sehemu ya umiliki wa viwanda vya JATU.

Kupitia kampuni ya JATU watanzania wanaweza wakaingiza kipato hata pasipo kuhusika moja kwa moja kwenye suala tu la uzalishaji. Bali kuhusika kwenye utumiaji pekee wa vyakula na bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ya JATU.

Hili kuweza kupata elimu na taarifa mbalimbali za uchambuzi wa kina endelea kutusikiliza kupitia DFM RADIO HAPA au pakua App yetu ya Dfm kwenye Google play store kutusikiliza live.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz