Je, unajua kuwa upekee wako ndio utofauti wako?

Umewahi kujiuliza kwanini umeumbwa John na si Hamisi au kwanini umeumbwa Asha na si Rose?. Kwa swali hilo tu kwanza utajua wewe ni wapekee sasa hatua ya pili ni kujua upekee wako upo wapi.

Upekee wa kijana ndio nguvu yake. Upekee ulionao ndio utofauti wako. Kitu chochote kinachoweza kukutofautisha wewe na watu wengine ndio kitu kinachoweza kukutambulisha wewe ni nani katika ulimwengu huu. Na katika hicho una uwezo wa kuwa unachotaka kuwa.

Vijana wengi wa leo wamekata tamaa kutokana na yale yanayowazunguka. Wapo wale ambao wamejikataa na kujiona hawafai mbele ya jamii. Kutana na Mwalimu Richard Mndala akitoa kwenye kipindi cha D-Youth katika muendelezo wa mada ya “Upekee wa Mtu”

“Tulikukuwa tunazungumzia kweli za msingi sana ambazo zinazungumzia upekee wa mtu kwa maisha ya kijana”-Mwalimu Richard

SOMA ZAIDI:

Kweli za msingi zinzozungumzia upekee wa mtu

  • Hakuna mtu anayeweza kushindana na upekee ambao Mungu ameuweka ndani yako.

Kamwe katika maisha usiwe na roho ya ushindani ya kutamani kuwa zaidi ya mtu mwingine. Kimsingi hakuna mtu anayeweza kuwa zaidi ya mtu mwingine lakini unaweza ukashindana na wewe mwenyewe wa jana.

Hakuna namna kubwa ya kupasha moto upekee wako nje ya maarifa. Kwenye zama hizi za taarifa unapaswa kujua ni taarifa gani unapaswa kuzipokea.

Kuna nguvu kubwa sana katika taarifa, taarifa ukiipata unaanza kutengeneza mtazamo ambao unakupa hamasa ya kufanya tendo la kitu Fulani na kuweza kudhihirisha kuwa hicho kitu kuwa kiko ndani yako na kutengeneza tabia.

HATUA ZA MCHAKATO WA TAARIFA

  1. Taarifa (Information)
  2. Mtazamo (Imagination)
  3. Hamasa  (Motivation)
  4. Tendo      (Action)
  5. Tabia (Habit)
  6. Shuhuda (Testimony)
  • Upekee wako huwa unaamua mtindo wa maisha unayoishi

Lazima mtu mwenyewe ajue kwanza anaishi maisha ya namna gani?, unavaaje, unakuaje? Vyote hivi vinaendana na upekee wako. Mungu anasema kuwa “nitakupa kufanana na wewe” Hakuna mtu ambaye ni kamili, kila mtu ana mapungufu na nguvu zake.

“Mungu anaposema nitakupa kufanana na wewe, ana maana atakuletea mtu ambaye atakuja kuziba mapungufu yako ili upekee na uzuri wako uonekane zaidi”-Alisema Mwalimu Richard.

Mwalimu Richard anasema mtindo wa maisha utolewa haswa na mafundisho kutoka kwenye vitabu vya Dini hasa biblia.

“Kuna mtu katika biblia anaitwa Daniel aliyetoka kwenye Taifa la Israel. Alipata kwenda sehemu ya ugenini yenye tamaduni yake na kukutana na mfalme na wanazuoni. Walitakiwa wanye divai na kula chakula alichoaandaa mfalme, Daniel alikataa kukocopy mtindo wa maisha wa watu wengine”-Mwalimu Richard.

Usishindane kuwa kama mtu Fulani, shindana siku zote kuwa kama wewe. Pambana siku zote uwe wa tofauti na mtu tunayemjua Yule wa jana anayekuwakilisha.

Kuendelea kusikiliza vipindi vingine mbalimbali vya Dfm radio, pakua App ya Dfm radio utusikilize moja kwa moja ili upate kuhabarika, kuelimika na kuburudika kwenye vipindi mbalimbali kama D-Business, D-Youth, D-Love, pamoja na vipindi vyote vya dini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz