Je imani ya nguvu upo nayo?

Hivi umewahi kufikiri kuna mtu anaweza kupangisha chumba kwa shilingi elfu mbili kwa mwezi? Kwa uhalisia najua utashangaa nini kinazungumzwa hapa. Ukijaribu kupiga mahesabu ya gharama za ujenzi wa nyumba yako na maisha jinsi yalivyo, hupati jibu kabisa na wala hutegemei kupangisha mtu kwa shilingi elfu mbili.

Ndiyo, kuna wapangaji wanapitia changamoto ngumu sana za maisha lakini mwenye nyumba atavumulia changamoto za watu wote? Sio wajibu wake. Lakini Wakati mwingine Mungu humchagua mtu mmoja na kumfanyia upendeleo fulani ili kumjengea ushuhuda kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Hii ni sehemu ya maisha ambayo mwimbaji Edson Mwasabwite aliyaishi baada ya wazazi wake kufariki. Alianza kujitegemea, akapata nyumba ya kupanga kwa shilingi elfu mbili kwa mwezi lakini hatahivyo hakuiwa rahisi kulipa kodi hiyo. Ni mangapi amaeyapitia mpaka anatoa wimbo wa “NI KWA NEEMA TU”? fuatilia visa na mikasa (hapa).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz