Huyu ndiye Mtumishi wa Mungu mwenye tuzo ya malkia wa Nguvu

Takwimu za usawa wa kijinsia katika ajira zinaonyesha kwamba kufikia mwaka wa 2014 Watanzania milioni 2.1 walikuwa wameajiriwa katika sekta rasmi , ikiwa ni pamoja na serIkalini na sekta binafsi, kwa mujibu wa kituo cha taifa cha takwimu.

Hata hivyo takwimu rasmi za serikali zinaonyesha pia kwamba zaidi ya 60% ya wanawake walio kati ya umri wa miaka 18 hadi 24 yaani million 13.9 wanajishughulisha na shughuli zisizo rasmi yaani biashara ndogondogo, kilimo na shughuli nyingine.

Jessica Mshama ni mwanadada mjasiriamali ambaye amejikita katika kuendesha biashara mbalimbali kama vile biashara ya nywele pamoja na maduka ya vyakula (Super Market). Licha ya kushughulisha katika biashara, Jessica ni mmoja kati ya mwanachama wa kundi maarufu la Muziki wa Injili lijulikanalo kama J Sisters, yeye akiwa ndio mdogo wa mwisho kwa akina dada hao.

Lakini pia Jessica amefanikiwa kutununikiwa tuzo ya Malkia wa nguvu ajaye 2019, katika kutambua mchango wa shughuli zake anazoziendeleza.

Kupitia kipindi cha D-Business kinachorushwa na Radio ya Mtandaoni (Online radio) ya DFM, Jessica kwa mara ya kwanza ameweka wazi uwezo wake wa kuendesha biashara huku akiwa anamtumkia Mungu kwa njia ya mahubiri na uimbaji.

Amesema kuwa licha ya kuwa mtumishi wa Mungu, wakati wote alikuwa ana ndoto ya kutaka kumiliki na kusimamia miradi na biashara mbalimbali huku hakusita kueleza kuwa moja ya biashara iliyokuwa kwenye ndoto yake ni pamoja na kumiliki biashara ya Urembo.

Maandiko matakatifu katika kile kitabu cha Hagai 2:8, Bwana anasema “Fedha ni Mali yangu na dhahabu ni mali yangu, Asema BWANA wa Majeshi” na usemi huu anauthibitisha mwanadada Jessica Mshama, licha ya kuwa anamiliki na kusimamia biashara mbalimbali, lakini anasema yeye bado ni mtumishi wa Mungu.

Akiwa mwanamke ambaye amefanikiwa pia kwenye ulingo wa Elimu, Jessica Mshama, ambaye amehitimu stashahada ya Usimamizi wa Biashara na baadaye shahada ya kwanza ya Fedha anaweka wazi siri zake za kufanikiwa katika

SIRI TANO ZINAZOMFANYA JESSICA AFANIKIWE

  1. Malengo (Focus)

Malengo ndio msingi mkubwa wa kuelekea kwenye kilele cha mfanikio makubwa. Jessica anasema tangu akiwa mdogo anasoma shule alikuwa na malengo ya kufanikiwa hasa katika upande wa kumiliki na kusimamia biashara kitu ambacho amekiria alianza kufanya akiwa shuleni.

Nakumbuka mara ya kwanza kuuza nywele nikiwa mwanafunzi, nilirudi nazo wakati nyumbani wakati wa likizo, mama akanicheka sana kwa sababu ni kitu ambacho kilikuwa kwangu mimi peke yangu, not anybody expected”-Alisema Jessica huku akiwa anacheka

  1. Usitumie kitu ambacho hauna

Jessica anasema vijana wengi, wanatumia mtaji, faida na nyenzo zote zinazotakiwa katika kuendeleza mtaji kwa tamaa. Kwake Jessica anaona haupaswi kutumia kitu ambacho hauna.

  1. Tafuta kujua (Seek knowledge)

Jessica anasema kwa kila kitu chochote unachotaka kufanya unapaswa kutafuta ujuzi au maharifa. Njia pekee ya kuweza kuliendeleza jambo Fulani na kufikia malengo ni kutafuta kujua.

  1. Kumtanguliza Mungu

Jessica ni mwanadada anayeunda kundi la kumsifu Mungu la J. Sisters, kwakwe anaona kuwa nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ni vyake, hivyo basi kazi yake ya kumsifu Mungu ni muongozo wa Maisha yake wakati wote.

  1. Kutoa Sadaka

Kila mmoja wetu anapaswa kutoa sadaka. Dini zote zinafundisha kutoa Sadaka. Nguzo kuu za Dini ni pamoja na kutoa Sadaka. Jessica anasema ili mtu aweze kufanikiwa hana budi kutoa Sadaka. Kwani kutoa Sadaka hakukupunguzii badala yake kunaongeza Baraka ya mambo yako.

Unaweza pia kusikiliza vipindi Mbalimbali vya D-Business kupitia radio yako ya Dfm hapa hapa ua kupitia tovuti yetu ya www.dfm.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz