D – Youth

Je, unajua kuwa upekee wako ndio utofauti wako?

Umewahi kujiuliza kwanini umeumbwa John na si Hamisi au kwanini umeumbwa Asha na si Rose?. Read More

Upekee wako ndo Utofauti wako

Vijana wengi wa leo wamekata tamaa kutokana na yale yanayo wazunguka. Wapo wale ambao wamejikataa na kujiona hawafai mbele ya jamii. Kumekuwa na wale wanaofikia hatua ya kulaumu na kukufuru kwanini alikuepo duniani. Huo ni upande mmoja ambao ni mgumu kwa kijana ambae anapita katika mazingira  magumu.

Tuje upande wa pili sasa kwa wale ambao hawapitii katika hali ngumu, hawa nao kuna changamoto ya kuiga kile au vile mwenzake anaishi. Wengi wamekua na maisha ambayo sio yao na kufikia hatua hata ya kuwa na maisha mawili. Maisha halisi na maisha ya mtandaoni vinakuwa ni vitu viwili tofauti kama maji na mafuta. Wewe kijana unaesoma waraka huu tambua thamani yako na upekee ulionao.

Umewahi kujiuliza kwanini umeumbwa John na si Hamisi au kwanini umeumbwa Asha na si Rose? Kwa swali hilo tu kwanza utajua wewe ni wapekee sasa hatua ya pili ni kujua upekee wako upo wapi. Kutana na Mwalimu Richard Mndalaakitoa semina kwa vijana wote kupitia DFM ndani ya kipindi cha D-YOUTH. Sikiliza kwa kubofya hapa chini.

Mwarobaini wa dhambi za Ngono kwa vijana Wapatikana

Imekua ni jambo la kawaida hasa kwa vijana wa sasa kufanya ngono wakidhani ni kwenda na wakati na kufikia kuona wale wasiofanya hivyo ni washamba au wanamatatizo kibaiolojia. Read More

Uthubutu wako upo wapi?

Kama kijana umewahi kujiuliza nguvu yako ya kuthubutu kufanya jambo ipo wapi? Huwa unapata muda wa kutafakari na kujifanyia tathimini kuhusu uwezo binafsi ulionao na jinsi unavyoweza kuutumia kubadilisha maisha yako? Pale unapogundua unaweza kufanya jambo fulani huwa unachukua hatua gani? Bado kuna ile hali ya vijana wengi kuona kwamba flani ndo anaweza kufanya jambo fulani, je, wewe unaweza kufanya nini?

Emmanuel Makwayani kijana ambaye amefanikiwa sana kwa sababu ya uthubutu wake. Yeye ni mwalimu lakini pia ni mwandishi wa vitabu. Moja ya kitu ambacho kijana wa kitanzania unatakiwa kujua ni unathubutu vipi? Maisha ya Makwaya yalikuwaje na tangu alipojitambua anaishije. Je kijana anatakiwa aishi kwa mtazamo upi ili afanikiwe. Unawezaje kufanya jambo kuwa unayetaka kuwa?

Sikiliza D-YOUTH upate madini mazito yatakayo kusaidia kuwa mtu wa kuthubutu. Bofya hapa

Kujitolea kwenye Ajira

Waswahili wanasema mchumia juani hulia kivulini. Vijana wengi leo wanapohitimu masomo yao hutegemea kupata ajira kwa haraka. Read More

Changamoto mtaji

Changamoto unazokutana nazo kwako ni fursa ama kikwazo? Kama ni kikwazo kwako unatatuaje? Kama ni fursa kwako unaitumiaje? Read More

Fursa katika kalamu

Kila ndege hupenda kutua katika mti aupendao, vilevile maji nayo hutiririka kwa kufuata mkondo. Read More

UREMBO NI AJIRA.

Kuajiriwa sio kikwazo cha kukwamisha ndoto ulizonazo kama mwanadamu. Mungu amemuumbia kila mwanadamu uwezo binafsi ndani yake na kila mtu ana kitu chake cha kipekee kinachomtofautisha na wengine. Read More

ROBERT MPEPA NDANI YA TASNIA YA  FASHION.

Wakati mwingine kwenye maisha unahitaji kubonyeza “button” sahihi ya kufungua maisha unayoyataka. Kushindwa jambo Wakati mwingine sio kwamba hulijui vizuri au una bahati mbaya, Wakati mwingine ni kwamba kuna jambo lako maalum ambalo hujaliona na badala yake unahangaika na lingine. Read More

AJIRA NDANI  YA KIPAJI.

Hivi una habari kuwa kipaji ni  uwekezaji  tosha wa Mungu ndani ya maisha ya mwanadamu. Kwa nini wengi hawajui uwezo walionao na kuutumia kufanya mambo makubwa na jinsi gani wanaweza kubadilisha jamii kupitia vipaji vyao? Read More

dfm.co.tz