D – Testify

Mapito ya maisha ya Bi Christina Kimani

Ukiwa kama binadamu unaweza kupitia mapito mbalimbali. Unaweza kupitia magumu mengi ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kukurudisha nyuma. Yote haya ni sehemu ya majaribu kama binadamu. Lakini wale waliopitia mapito hayo na bado hawakumuacha Mungu basi walipata kuiona kesho yao.

Kutana na shujaa wa siku Bi. Christina Joseph Kimani maarufu sana kwa jina la mama Kavemba kwenye kipindi cha D-Testify akizungumza moja kwa moja na muendesha kipindi Aaron D.  Ilan.

SIKILIZA ZAIDI

Mwanzo wa safari ya shida na Raha ya Bi christina

Safari ya maisha ya mapito kwa mama Kevemba ilianza miaka ya 70 kama mwenyewe anavyodai. Maisha yake ya vikwazo yalikuwa yanampa simanzi mara kwa mara kabla ya kuamua kumrudia Mungu wake.

Bi. Christina alianza maisha ya kumtumikia Mungu akiwa bado hajaokoka licha ya kukiri kuwa mahubiri ya watumishi wa Mungu mbalimbali yalimpa hamasa na kuamua kuokoka mwaka 1978 katika kanisa la Mwenge.

Sababu kubwa ya yeye kuokoka ni kutokana na ajali ya pikipiki aliyowahi kuipata katika miaka hiyo ya 70. Katika ajali hiyo ya pikipiki,mama Kavemba alikiri kumpoteza mume wake kipenzi kwenye ajali hiyo.

“Tulikuwa kwenye pikipiki mimi na baba watoto wangu, yeye alifariki hapo hapo kwenye ajali. Kwakweli mimi Mungu alinisadia, nikapelekwa Muhimbili kwa matibabu”-Bi Christina alisema

Bi. Christina anasema mara baada ya kupata matibabu kutoka Muhimbili alipata kusikia maneno ya watu mbalimbali ambao walikuwa wanakiri na kushuhudia kuwa Yesu anaponya. Hapa ndipo ilipoanza safari ya mama Kavemba kumpokea Yesu.

Licha ya kuwa Bi. Christina kudharau mara kwa mara maneno ya ushuhuda juu ya Yesu anaponya, anasema lakini hakusita kuyatilia maanani maneno hayo na baadae kuanza kuyafanyia kazi.

Maisha ya Wokovu ya Bi. Christina

Maisha ya wokovu ya Bi Christina anasema ni ya furaha na upendo sana hasa kwa mchungaji wake pamoja na mama mchungaji. Maisha haya aliyafurahia sana licha ya kukiri kubadili kanisa alilokuwa akisali hapo awali.

Katika maisha yake ya wokovu Bi Christina amekuwa akilitumikia kanisa hasa pale alipobarikiwa kupata nafasi ya kuwa karani wa kuhesbau sadaka za kanisa (cashier).

Bi Christina anasema maisha ya wokovu kwa wakati huo yalikuwa ya kujitoa kwa hali ya juu.

Kwa sasa Bi Christina ni mwalimu wa masomo ya neno la Mungu akitoa mafundisho mbalimbali.

Kuwa wa kwanza kusikiliza  kipindi chako bora cha D-Testify kupitia deep fem radio ili uweze kupata shuhuda mbalimbali. Sikiliza kupitia mtandao au kwa kupakua App ya deep fm kwenye simu yako. TUSIKILIZE HAPA. Bofya HAPA chini kusikiliza kipindi hiki.

Bibi wa miaka 87 katika maisha ya wokovu

Suala la kumtumikia Mungu ni la kila mwanadamu aliyekuwa katika Ulimwengu huu. Maisha ya kumtumikia Mungu daima yakufanya kuwa karibu na Mungu Katika kila jambo. Read More

Maisha baada ya Utajiri

Safari yoyote huwa na mwanzo wake lakini kuna wale ambao hawafiki mwisho, wengine wanabadili uelekeo na wengine humaliza vizuri safari. Kwenye maisha kuna kitu kinaitwa kujiongeza. Katika kujiongeza huko kuna kutumia njia za mkato au njia ya moja kwa moja ili kufanikisha kile ulichodhamiria. Alex William Kishimba ni mchungaji ambae alipitia katika maisha ya utajiri lakini baadae mambo yalibadilika.

Akiongea na DFM mchungaji Alex hakusita kufunguka na kueleza namna maisha yalivyokuwa matamu kwake na pale ambapo yalibadilika kwa ghafla na chanzo chake nini, katika pitapita yake alisema kuna sauti ambayo alikua anaisikia ikiongea nae kila mara. Sauti hiyo ilikua ikimnyima amani kabisa.

Kwa mwendelezo wa simulizi hii sikiliza kipindi cha D-TESTIFY ili kupata data kamili ya nini kilimkumba mchungaji huyo na ilikuaje. Baki hapa kwa uhondo huu.

Majaribu ni Mtaji

Majaribu yanapokuja yanakufanya ushindwe kusonga mbele au ndo yanakupa nguvu ya kusonga mbele? Read More

Je imani ya nguvu upo nayo?

Hivi umewahi kufikiri kuna mtu anaweza kupangisha chumba kwa shilingi elfu mbili kwa mwezi?  Read More

Sakata la Kujiua

Wakati changamoto zinapowasonga watu na kufawanya wasione mwelekeo wowote, wengi huona suluhisho kubwa ni kuondoka duniani hivyo hupelekea kitendo cha kujitoa uhai wao. Read More

 MADAWA YA KULEVYA NA SUMU.

Kutana na Producer Geofrey ajulikanae kwa jina la PG katika kipindi cha D-TESTIFY ndani ya studio za DFM akielezea namna madawa ya kulevya yalivyo muathiri, lakini pia kuponea chuchupu kifo baada ya kula chakula chenye sumu. Nini kilitokea wakati madaktari walikua wamekata tamaa wakijua amefariki.

Read More

Matatizo katika Uchumba

Umewahi kujiuliza juu ya jina ulilopewa lina maana gani na sababu ipi ilipelekea wewe kupewa jina hilo? Wapo watu wengi ambao wanakubali kuitika wanapoitwa flani lakini hawajui hata chanzo ni nini. Kuna story moja ya kusisimua sana kuhusu muimbaji wa nyimbo za injili ajulikanae kwa jina la Siza Mwampamba DFM ilipata historia yake tangu kuzaliwa kwake mpaka uchumba wake na kuolewa kwake.

Mama yake alimwambia wakati wa ujauzito wake ilipofika miezi nane ya ujauzito mtoto akafariki tumboni. Madaktari wakaanza harakati za kumuokoa mama ili asipate madhara, ndipo wakampeleka chumba cha upasuaji na kumpasua kutoa mtoto. Wakati madaktari wakidhani watatoa maiti walishangaa wanatoa mtoto mzima tena anacheka badala ya kulia. Hivyo ndivyo Siza alivyokuja duniani.

Alipofikia umri wa kuolewa na kupata mchumba, akakumbana na changamoto nyingine hadi kupelekea ndoa yake kusimamishwa kwa muda. Je, watamani kujua nini kilitokea? Fuatilia kisa hiki kupitia D-TESTIFY kwa kubonyeza (hapa).

 

 

About DFM

Deep Radio FM is an online radio which is dedicated to inspire, motivate and amuse listeners through an eclectic mix of Christian music, educational and social affairs programs and services. DFM is the forum that allows all people from all works of life to benefit from deep knowledge on issues that can promote positive social change and transform people’s destinies but typically lack media access and continuity. It is registered in Tanzania with having radio license from TCRA

Our vision: To provide our esteemed listeners with deep and exceptional divine services in the world of digital content.

Our mission: To produce compelling content that inspires, motivate and encourages people to have purposeful relationship with God and have their Destinies divinely transformed.

Our story: Deep FM is basically originated from Luke 5:4 which says, ‘When He had finished speaking, He said to Simon, “Launch out into the deep, and let down your nets for a catch.”

Our Values:

  • We Trust in God. Our faith, trust, and hope is in Christ. God’s Word guides our decisions, refreshes us, and creates within us an unshakable faith. Our dependence on God is reflected in our commitment to prayer.
  • We Learn, Improve, and Grow. We challenge and stretch ourselves, each other and the whole Deep Community to realize the full potential God has graced us with.
  • We create an Extraordinary Impact. We serve an extraordinary God who deserves our all. He allows us to create, produce and share contents with His life-changing message.
  • We are Passionate, Creative, and we do have fun while living a purpose driven life
  • Innovative ideas and solutions, individual initiatives, and team work makes our work and lives more interesting.
  • In His Strength. It’s not about us

Mtoto aliyepotea kupatikana

Pumzi ambayo unayo ni sababu ya mapenzi ya Mungu, afya ulionayo pia ni sababu ya ulinzi wa Mungu. Read More

Kodi ya Shilingi elfu mbili kwa mwezi bado ilikuwa ngumu kuipata

Hivi umewahi kufikiri kuna mtu anaweza kupangisha chumba kwa shilingi elfu mbili kwa mwezi? Read More

dfm.co.tz