D HITS

Msikilize Producer wa Angel Benard wa “Siteketei”

Kwenye kazi za muziki kuna kitu kinaitwa lebo (label), wanamuziki wanajua naongelea nini hapa. Read More

Uhalisia wa Maisha ya Muziki wa Injili

Msanii yeyote katika jamii anasimama kama kioo cha jamii husika. Haijalishi ni msanii wa tasnia gani iwe muziki, sinema na hata fani nyingine. Wote uwakilisha dhima kuu tatu kuelimisha, kuhabarisha na hata kuburudisha. Japo ufikishaji ujumbe kwa jamii utofautiana kulingana na fani husika ya msanii husika.

Kwa kipindi cha karibuni wasanii wa nyimbo za Injili wameonekana kuja juu katika muziki huo wa Injili Sanaa hasa wasanii wanaoimba mmoja mmoja (Solo artist). Hii ni kutokana na jamii sasa kuanza kuilewa vizuri Sanaa hii hasa katika kulitangaza neno la Mungu.

Lakini kwa namna moja ama nyingine ipo mitazamo ya wengi juu ya waimbaji na wasanii wa nyimbo za injili. Hasa wenye majina makubwa.

DFM imepata muda wa kuongea na wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili kama vile Solomoni Mukubwa, Ivan Moshi kuhusu mambo mbalimbali yanayowagusa kwa namna moja ama nyingine. Baadhi ya mambo hayo ni kama yafuatayo.

SOMA ZAIDI

Mitazamo mbalimbali ya wasanii wa muziki wa Injili

  1. Kuhusiana na kufanya Video nje ya nchi

Dfm imeongea na wasanii mbalimbali wa muziki wa injili kuhusiana na suala hili ambalo limekuwa na maswali mengi sana. Moja ya wasanii waliopta kuzungumzia siuala hili ni Ritha Komba.

kwenye mazungumzo na DFM, Ritha Komba anasema sio lazima sana kufanya video nje ya nchi. Na ili utoke sio lazima ufanye video yako nje ya nchi bado unaweza kufanya hapa hapa nyumbani na ukatoka.

Mimi nachoweza kusema ni kuwa chochote unachoweza kukifanya kwa mahali popote kwa kiwango kizuri kitakubalika, kutoka ni mpango wa Mungu haijalishi umeenda sehemu gani?”-Ritha Komba

  1. Vitu gani wanapaswa kufanya ili kufanikisha Malengo yao ya Muziki.

Christina kutoka Kubamba Fm ya nchini Kenya. Amasema wasanii wanapaswa kufanya matamasha mengi pamoja na nyimbo nyingi za kushirikiana na wasanii mbalimbali wa muzikiwa Injili. tena kutoka pande mbalimbali ikiwezekana hata nje ya nchi kwa ajili ya kujitangaza na kuongeza mashabiki.

  1. Kuhusu maisha ya wasanii wa muziki wa Injili.

Watu wengi wamekuwa na dhani ya kutabiri maisha ya watu walio maarufu. Wapo wanaosema kuwa maisha ya wasanii wa muziki wa injili ni makubwa na ya kifahari sana. Kwa kutaka kujua hilo na kutoa ukakasi uliopo baina ya raia na wasanii, DFM imefanya mazungumzo na Solomon Mkubwa muimbaji wa nyimbo za injili.

Yeye ametetea hoja hiyo kwanza kwa kueleza yeye ni nani lakini pia alizama ndani kidogo kueleza maisha yake tangu anazaliwa mpaka hapo alipo.

“kama tuko hapa tunafanya hii kazi na kwa ajili ya utukufu wa Mungu, watu wanatuonaga kwa Tv wanadhani sisi ni mabilionea, sisi tunataka kuwapa Imani watu”-Solomon Mkubwa

Ndugu Solomon aliwahi pata matatizo katika maisha yake na hakusita kueleza nini kilimkumba mpaka kufikia hatua ya kuwa na mkono mmoja wakati alikuwa mzima kama wewe. Sikiliza story hii ya Solomon ndani ya DFM kwenye kipindi cha D-HITS. BOFYA HAPA kusikiliza.

 

Kemea Pepo

Moja ya vitu ambavyo watu wengi wanaangalia kwenye nyimbo za injili ni maudhui ya wimbo huo. Kumekuwa na mijadala tofauti tofauti kuhusu nyimbo za injili na maudhui yake. Ukiacha maudhui hayo kuna mavazi pia ambayo huwa wainjilishaji ama waimbaji wa nyimbo za injili mengine yamekuwa maswali kwa watu, mengine yamekuwa majibu lakini mengine yamekuwa sintofahamu.

DFM katika kutafuta majibu hayo ilikutana na Emmanuel Mgaya ajulikanae kwa jina maarufu la Masanja Mkandamizaji. Masanja alitoa ushirikiano mzuri kujibu maswali aliyoulizwa na pia kueleza namna wimbo wake ulivyopokelewa na jamii. Wimbo wake unajulikana kwa jina la KEMEA PEPO na amesema yeye amefurahi kwa sababu wimbo wake umekuwa tiba.

Je, watamani kujua tiba hiyo ni ya aina gani? Sikiliza D-HITS mwenyewe usisubiri kusimuliwa uhondo huu wa kumsikia Masanja akitema cheche zake kuhusu tasnia hii ya muziki wa injili. Bofya hapa chini kwa kusikiliza.

Uchungaji na Uimbaji

Kushika mambo mawili sio tatizo japo inaweza kuwa changamoto kwa baadhi ya watu hasa pale ambapo yote yanaonekana kuwa na nguvu. Read More

Ukongwe ni Uhodari

Ladha ya vitu kongwe je, huwa inakuwa na thamani ileile ukisikiliza wakati ukiwa umeshapita? Labda nikukumbushe ule msemo wenzetu wanasema “old is gold”. Sio mbaya mara moja moja kusikiliza vitu kongwe hasa katika tasnia ya uimbaji ni kitu ambacho kinakukumbusha wapi tumetoka. Kanisa la TAG Mwenge waliongea na DFM kutupasha habari kuwa kwaya yao imetimiza miaka 40 sasa.

Hivi unakumbuka vifaa vya muziki vilivyokuwa vinatumika zamani kutoa ala mbalimbali katika kuweka vionjo vya muziki? Mpangilio wa sauti ambao unasikika ukilinganisha na huu wa sasa unaona kuna tofauti gani iliyopo. Umuhimu wa kubadiisha style ama mitindo ya uimbaji upo wapi?

D-HITS ilipata kuzungumza na Imani Kwaya ambayo imetimiza miaka 40 na kuweza kutoa historia yao wapi walianza mpaka hapo walipo. Kwa kujifunza zaidi sikiliza (hapa)

Upako wa Kwaya

Waimbaji wengi wa nyimbo za injili inaonekana wametokea kwenye kwaya. Wengine pia huonekana wamejitambua wana vipaji tangu wakiwa wadogo. Read More

Waimbaji wa nyimbo za injili kuhamahama makanisa

Kile kitendo cha mtu kutokuwa na kanisa maalum ambalo anafahamika hapo ndo nyumbani kwa baba wa kiroho, ni kitendo ambacho kinafanya mtu huyo asieleweke yupo kwenye msimamo gani na anatafuta nini. Read More

Fursa na Tamufo

Kama bado ulikuwa hujui kwenye uimbaji wa nyimbo za injili neema imekuwa kubwa. Read More

Injili na Muonekano

Muonekano wako unakutambulisha kama nani mbele ya wanaokuzunguka? Read More

 UNAKUMBUKA UMETOKA WAPI?

Hatua unazopiga kuelekea kule unapotamani kufika ni moja ya maendeleo katika kile unachokifanya. Umewahi kujiuliza kipi umefanya, wapi umetoka, wapi ulianguka, nani alikuunga mkono, unaelekea wapi na umefika wapi? Atosha Kisava ni muimbaji wa nyimbo za injili ambaye amepitia mchakato mrefu kufika hapo alipo.

Atosha amesema yeye mpaka amefika pale alipo sasa kuna mahali alitoka. Akiongea na DFM amesema safari yake ya kuelekea kwenye muziki w Read More

dfm.co.tz