Bibi wa miaka 87 katika maisha ya wokovu

Suala la kumtumikia Mungu ni la kila mwanadamu aliyekuwa katika Ulimwengu huu. Maisha ya kumtumikia Mungu daima yakufanya kuwa karibu na Mungu Katika kila jambo. Kila mmoja wetu huwa anafundishwa kuishi katika maisha ya wokovu ambayo yanampendeza Mungu. Japo nkumekuwa na malalamiko mengi dhidi ya walokole wa sasa.

Shida iko wapi kwa walokole wa leo? Moja ya vitu ambavyo inatakiwa kujiuliza nini chanzo cha wengine kurudi nyuma? Bibi Anna Lota “Lota” ana umri wa miaka 87 na amekaa kwenye maisha ya wokovu kwa kipindi cha miaka 40. Dfm kupitia kipindi chake cha D-Testify imepata muda wa kuzungumza nae kwa undani Zaidi kuhusu maisha ya wokovu ya mwanadamu.

SOMA ZAIDI:

Kwanza tupaswa kufahamu nini maana ya Wokovu?

WOKOVU, kwa maana ya jumla ni kuondolewa hali isiyopendeza au ya hatari kabisa.

Katika Ukristo, wokovu maana yake ni kwamba, katika mfululizo wa matukio ya Dunia hii, Mungu anawakomboa binadamu kwenye dhambi zao na kutoka matokeo yake katika Maisha ya Duniani na katika Uzima wa Milele.

Maisha ya Wokovu ya Bibi Anna Lota “Lota”

Maisha ya wokovu ya bibi Lota yalianza miaka 40 iliyopita huko nyuma. Amasema alianza maisha ya kumtumikia Mungu akiwa mtumishi wa hospitali ya Muhimbili na baadaye kuhamia kwenye kanisa lao jipya la Kigogo, Jijini Dar es salaam. Katika kipindi cha maisha yake yote ya wokovu Bibi Lota amefanikiwa kudumu ndani ya kanisa  moja mpaka sasa.

Katika maisha yake yake, Bibi Anna amegundua utofauti wa wokovu wa sasa na waliopita. Bibi Anna anasema

  1. Wokovu wa zamani ulikuwa unafuata misingi ya Dini

Kwa mujibu wa Bibi Lota anasema kipindi cha zamani, walikuwa unafuata misingi ya wokovu ikiwa ni pamoja na kuwa na hofu ya MUNGU. Bibi Lota anasema vijana wengi walio kwenye dini kwa sasa hawana hofu ya Mungu, hivyo wao kama waliowatangulia kwenye maisha ya wokovu wanapaswa kuwaombea vijana wadumu, waishi na wasimame kwenye maisha yanayompendeza Mungu.

  1. Wokovu wa zamani ulikuwa unazingatia misingi ya ndoa

Bibi Anna anasema wokovu wa zamani ulikuwa unalenga kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Akina mama walikuwa wanazitunza ndoa zao kwa kufuata misingi ya Dini. Bibi Lota anasema nyumba inatakiwa kuwa na mama aliyeokoka.

  1. Mavazi ya kanisani ni ya heshima Zaidi

Bibi Lota anasema neno la Mungu linatuambia tuwe katika msimamo mzuri kwa mavazi na mienendo yetu. Suala la mavazi anasema katika kipindi chao mtu alikuwa hawezi kuvaa mavazi ambayo hayampendezi Mungu.

Tumia muda wako kumsikiliza bibi huyu ambaye ambaye ameonyesha ukomavu kwenye kumtumikia Mungu kwa Zaidi ya miaka 40. sikiliza D-TESTIFY hapa hapa. Najua ukisikiliza utajifunza vingi sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz