Je, unazijua faida ya kusajili biashara zako?

Kufanya biashara ni moja ya maamuzi sahihi kwa wengi lakini wengi hawayafanyi haya maamuzi kwa usahihi. Kwa lugha nyingine wanafanya biashara sahihi lakini wanashindwa kuzingatia taratibu sahihi ambazo zinalenga kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara zao.

Mtu yeyote anaweza kuamua kuendesha biashara kwa ajili tu ya kutoa bidhaa au huduma kwa mtu mwingine ili kutengeneza faida wakati kusajili biashara kwenye mamlaka husika sio hitaji muhimu katika kukamilisha miamala ya biashara bali ni chaguo sahihi kwa mjasiriamali kutokana na sababu anuwai.

 

Faida 5 za kusajili biashara au kampuni yako

  • Urahisi katika kufanya biashara na watu wa ndani na nje ya nchi

Kuwa na biashara au kampuni iliyosajiliwa inakupa urahisi kufanya biashara na wadau wa ndani na nje ya nchi. Washiriki wenza wengi wa biashara uwekeza kwenye biashra inayoendeshwa kwa kanuni na sheria ili kuweka mazingira mazuri ya kibiashara.

  • Kutambulika na Mamlaka/Serikali

Unaposajili biashara au kampuni yako inakupa fursa kubwa kuweza kufanya shughuli zako za kibiashara kwa uhuru na kutambulika popote unapoenda kwenye eneo husika.

  • Kupata mikopo

Unapoomba mkopo wowote wa kibiashara unahitajika kuthibitisha biashara yako unayoifanya. Wawekezaji watataka kuona usajili wa biashara au kampuni yako.

  • Sifa nzuri kwa wateja wako.

Mteja au mwekezaji mpya katika biashara yako atataka kujua uhalali wa uwepo wa biashara au kampuni yako. Unaposajili kampuni yako unampa mteja wako fursa ya kufanya biashara ama kuwekeza kwa uhuru kwenye biashara yako.

  • Uwezo wa kuajiri wafanyakazi.

Kusajili kampuni au biashara kunakupa fursa ya kuajili wafanyakazi wa muda mrefu kwenye kampuni au biashara yako pamoja na kuwalipa kutokana na kanuni za nchi.

  • Kutambulika kwa biashara yako kwa kiwango cha juu.

Kampuni au biashara iliyosajili inakupa wigo wa kujitangaza popote pale kwa uhuru. Usiposajili kampuni hauwezi fanya matangazo kwa kiwango cha juu ili kuweza kukuza jina la biashara (Brand awareness).

  • Kupata akaunti ya Benki ya biashara.

Unahitaji kutoa uthibitisho wa usajili wa kampuni au biashara yako ili uweze kupata akaunti ya benki ya biashara. Akaunti ya baishara ya benki ni muhimu sana kwa mfanya biashara ili aweze kutofautisha shuguhuli zake za binafsi za kibenki na zile za biashara.

Usajili wa biashara ni wazi unaweza kutoa faida chanya kwa kampuni, nchini Tanzania sasa unaweza sajili kampuni yako kwenye mamlaka husika (BRELA) kwa njia ya mtandao

Hili kuweza kupata elimu na taarifa mbalimbali za uchambuzi wa kina endelea kutusikiliza kupitia DFM RADIO HAPA au pakua App yetu ya Dfm kwenye Google play store kutusikiliza live.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

dfm.co.tz