marondo sebastian

Huyu ndiye Mtumishi wa Mungu mwenye tuzo ya malkia wa Nguvu

Takwimu za usawa wa kijinsia katika ajira zinaonyesha kwamba kufikia mwaka wa 2014 Watanzania milioni 2.1 walikuwa wameajiriwa katika sekta rasmi , ikiwa ni pamoja na serIkalini na sekta binafsi, kwa mujibu wa kituo cha taifa cha takwimu.

Hata hivyo takwimu rasmi za serikali zinaonyesha pia kwamba zaidi ya 60% ya wanawake walio kati ya umri wa miaka 18 hadi 24 yaani million 13.9 wanajishughulisha na shughuli zisizo rasmi yaani biashara ndogondogo, kilimo na shughuli nyingine. Read More

Mchango wa Mahusiano kwenye Sanaa ya Muziki

Mahusiano uchukua nafasi kubwa sana katika maisha ya binadamu. Kwa namna moja ama nyingine suala la Mahusiano linaweza kuwa na matokeo chanya lakini wakati mwingine linaweza kuleta matakeo hasi kutoakana na jinsi wahusika watakavyolichukulia.

Ni jambo la kawaida kwa siku za hivi karibuni kuona kuwa baadhi ya wasanii wa Muziki wa Bongo Flava na hata wale kutoka tasnia nyingine za burudani wakiwa wanatumia mbinu ya mahusiano katika kuwasilisha Sanaa zao, maarufu kama “Kiki” kama vijana wa mjini wanavyosema.

Kupitia kipindi cha D-Love kinachorushwa na Radio ya Mtandaoni (Online Radio) ya DFM, msanii wa kizazi Bongo Flava, Luminaly anasema yeye haamini suala la mahusiano kwenye kazi zake za muziki licha yay eye kuwa kwenye mahusiano kwa Zaidi ya miaka 10.

Luminaly anasema unapokuwa msanii, wasichana wengi watakuwa wanakufuata lakini kwake changamoto hiyo anajitahidi kuikwepa akiamini kuwa kutumia mahusiano kama sehemu ya kick kuzipeleka kazi zake mbele sio njia sahihi ya kuwa na maisha marefu kwenye Sanaa.

kinachokuja haraka kinaondoka haraka, na kinachokuja taratibu kinaishi, ukitumia kiki utakuja kweli, tutakusikia, tutakufahamu lakini mwisho wa siku ni kama Upepo, unapita”-Alisem Luminary

Mchango wa Mahusiano kwenye Sanaa ya Muziki

Wapo wasanii ambao wao uona kuwa suala la mahusiano linaweza kuleta mchango chanya katika kazi zao za Sanaa. Wengi wao ndio ambao utumia mahusiano kama sehemu ya kujitangaza hasa pale wanapokuwa wanakaribia kutoa kazi zao mpya.

Kwa Luminary kwake ni tofauti ambaye licha ya kuwa kwenye mahusiano kwa Zaidi ya miaka kumi tena kwa mtu ambaye ana nafasi ya kufahamika, hajawahi kutumia nafasi ya mahusiano katika kuzitangaza kazi zake za Sanaa.

Suala la kutumia mahusiano kwenye Sanaa (Kiki) limekuwa gumzo sana nchini kutokana na wimbi kubwa la wasanii kuona kama ndio njia pekee inayoweza kufanya kazi zao ziwe juu.

Changamoto wanazozipata wasanii kwenye mahusiano.

Licha ya wimbi kubwa la wasanii kuona kuwa mahusiano yanaweza kutumika katika kuzitangaza kazi zao, lakini pia huwa wanapitia changamoto mbalimbali katika suala zima la mahusiano

 

  1. Muda

Luminary anasema yeye kama yeye anaona mahusiano yanaweza kukufanya ushindwe kutumia muda wako vizuri hasa ule muda ambao ulipaswa kuutumia katika kufanya kazi za Sanaa, na unajikuta kuwa unatumia muda huo kwa ajili ya kutunza mahusiano yako.

 

  1. Wimbi kubwa la wanawake ambao huwatafuta mara kwa mara

Luminary anakiri kuwa suala la umaarufu wakati mwingine linaleta changamoto kubwa kwa jamii. Anasema Iiafikia wakati huwa wanajikuta wanatafutwa na wanawake tofauti tofauti mara kwa mara na kama hawatakuwa makini wanaweza kujikuta wanapoteza malengo ya kazi zao za Sanaa.

 

Si kila mtu anapenda kuweka wazi mahusiano yake, wapo wasanii ambao hutumia mahusiano hasa na wanawake ambao maarufu katika mbinu mojawapo ya kujijenga kikazi Zaidi, lakini wapo ambao wanaona kuwa kutumia njia ya mahusiano ni kama kuharibu kazi na jina ambao amelijenga kwa muda muda Fulani.

 

Je unawafahamu Mke Mwema Group?

Mke Mwema ni kundi la wanawake walioko katika agano la ndoa ambalo lilianzia katika facebook na hatimaye kuwa jeshi kubwa ambalo limegusa maisha ya watanzania wengi kwa namna ya kipekee sana. Read More

Mke Mwema Day 2018

Mke Mwema ni kundi la wanawake walioko katika agano la ndoa ambalo lilianzia katika facebook na hatimaye kuwa ‘jeshi kubwa’ ambalo limegusa maisha ya watanzania wengi kwa namna ya kipekee sana.

TOFAUTI KATI YA MKE NA MWANAMKE.

Moja ya vitu ambavyo watu wengi tunashindwa kuelewa au kujua ni pale ambapo tunafananisha mke na mwanamke kuwa kitu kimoja. Siri iliyojificha ndani ya mke ambayo inaleta tofauti na mwanamke sasa yawekwa wazi na Dokta Love, ndugu Sylvester Paul ambae ametoa nondo nyingi kuhusu mwanamke na mke. Read More

UREMBO NI AJIRA.

Kuajiriwa sio kikwazo cha kukwamisha ndoto ulizonazo kama mwanadamu. Mungu amemuumbia kila mwanadamu uwezo binafsi ndani yake na kila mtu ana kitu chake cha kipekee kinachomtofautisha na wengine. Read More

Je? Unajua unaweza kumiliki kiwanda kwa sh. 2500/=?

Ile ndoto ya kumiliki Kiwanda kwa kila Mtanzania ni wazi si dhana ya nadharia tu bali wapo wanaoitumia fursa hiyo. Read More

UTUMBO ULIOJIKUNJA KUPONA BILA TIBA

Wakati wewe umekaa na kukumbatia tatizo ulilonalo, kwa wengine hiyo ni fursa ya kupeleka matatizo waliyonayo kwa Yesu. Yesu hana historia ya kushindwa isipokuwa tu watu wengi hawana tabia ya kumkimbilia na kumtegemea. Read More

MKRISTO NA MIPANGO.

Akili ya kujiongeza ni moja ya kitu ambacho kinawasaidia wengi sana, hata kama umeokoka na umejazwa Roho mtakatifu sio dhambi kuwa na akili ya kujiongeza. Imezoeleka sana kuona kwamba waliookoka ni choka mbaya kimaisha, “hahahahahah” pole sana, acha kupotea na kujidanganya. Ishi kwa mipango halafu utaona  jinsi maisha yako yatakavyobadilika. Read More

 UNAKUMBUKA UMETOKA WAPI?

Hatua unazopiga kuelekea kule unapotamani kufika ni moja ya maendeleo katika kile unachokifanya. Umewahi kujiuliza kipi umefanya, wapi umetoka, wapi ulianguka, nani alikuunga mkono, unaelekea wapi na umefika wapi? Atosha Kisava ni muimbaji wa nyimbo za injili ambaye amepitia mchakato mrefu kufika hapo alipo.

Atosha amesema yeye mpaka amefika pale alipo sasa kuna mahali alitoka. Akiongea na DFM amesema safari yake ya kuelekea kwenye muziki w Read More

dfm.co.tz