Joshua Wenceslaus

Je imani ya nguvu upo nayo?

Hivi umewahi kufikiri kuna mtu anaweza kupangisha chumba kwa shilingi elfu mbili kwa mwezi?  Read More

Uthubutu wako upo wapi?

Kama kijana umewahi kujiuliza nguvu yako ya kuthubutu kufanya jambo ipo wapi? Huwa unapata muda wa kutafakari na kujifanyia tathimini kuhusu uwezo binafsi ulionao na jinsi unavyoweza kuutumia kubadilisha maisha yako? Pale unapogundua unaweza kufanya jambo fulani huwa unachukua hatua gani? Bado kuna ile hali ya vijana wengi kuona kwamba flani ndo anaweza kufanya jambo fulani, je, wewe unaweza kufanya nini?

Emmanuel Makwayani kijana ambaye amefanikiwa sana kwa sababu ya uthubutu wake. Yeye ni mwalimu lakini pia ni mwandishi wa vitabu. Moja ya kitu ambacho kijana wa kitanzania unatakiwa kujua ni unathubutu vipi? Maisha ya Makwaya yalikuwaje na tangu alipojitambua anaishije. Je kijana anatakiwa aishi kwa mtazamo upi ili afanikiwe. Unawezaje kufanya jambo kuwa unayetaka kuwa?

Sikiliza D-YOUTH upate madini mazito yatakayo kusaidia kuwa mtu wa kuthubutu. Bofya hapa

Nguvu inayopingana na Mungu

Moja ya vitu ambavyo wengi wanadhani ni kazi kubwa ya kumfurahisha Mungu ni ile hali ya kutumia nguvu nyingi kukemea mapepo. Read More

Fikra zilizo Angavu

Unapoona jalala unapata fikra gani? Takataka na mabaki ya vitu mara nyingi huonekana kama vitu visivyofaa kwa matumizi ya aina yoyote. Read More

Mahusiano Nje ya Utaratibu

Mashine ni kifaa chochote ambacho hutumika kurahisisha kazi. Mfano kisu ni mashine ambayo hutumika kurahisisha kazi ya kukatakata vitu kama vile nyama, nyanya, matunda n.k. Read More

Upako wa Kwaya

Waimbaji wengi wa nyimbo za injili inaonekana wametokea kwenye kwaya. Wengine pia huonekana wamejitambua wana vipaji tangu wakiwa wadogo. Read More

Sakata la Kujiua

Wakati changamoto zinapowasonga watu na kufawanya wasione mwelekeo wowote, wengi huona suluhisho kubwa ni kuondoka duniani hivyo hupelekea kitendo cha kujitoa uhai wao. Read More

Kujitolea kwenye Ajira

Waswahili wanasema mchumia juani hulia kivulini. Vijana wengi leo wanapohitimu masomo yao hutegemea kupata ajira kwa haraka. Read More

Kukata Tamaa

Ni vitu vingapi umewahi kupoteza maishani mwako na kusababisha furaha yako kupotea? Ni mara ngapi umekuwa ukifeli katika maisha yako na kufikia kukosa tumaini la maisha? Read More

Tanzania ya Viwanda ni fursa adhimu ya Ajira

Tatizo la uwepo wa ardhi duni isiyo na rutuba ni wazi kunachochea upatikanaji finyu wa malighafi za uzalishaji. Hii ni fursa kwa jamii kutafuta njia mbadala ya kuendelea kuitunza ardhi kwa ajili ya kilimo endelevu chenye manufaa kwa viwanda.

Uwepo wa Sera ya uchumi wa Viwanda nchini ni wazi uzalishaji wa mali ghafi unapaswa kukua kwa kiwango cha hali ya juu sana. Ikizingatiwa sekta ya kilimo ndio chachu ya ukuaji wa viwanda.

Guavay ni kampuni ya Kitanzania iliyoanzishwa na baadhi ya vijana wa kitanzania maalumu kwa ajili ya kutengeneza na kuzalisha mbolea ya asili ya mimea aina ya Organic iitwayo “Hakika Organic Fertlizer”. inayotokana na mabaki ya matunda, mbogamboga na mimea.

Kwanini Guavay waliamua kutengeneza Mbolea ya Asili?

Sababu kuu ya kuamua kuja na mbolea ya asili ni kupotea kwa rutuba kwa ardhi ya Tanzania kulikochangiwa na;

  • Matumizi mabaya ya ardhi
  • Kutotumia mbinu sahihi za kilimo
  • Kutumia Mbolea ambazo zinachosha udongo

Licha ya upatikanaji mgumu wa Malighafi Guavay inapitia hatua kadhaa katika mchakato wa uzalishaji  wa mbolea ya Organic.

  • Ukusanyaji wa takataka zenye uwezo wa kumeng’enywa na wadudu (Bakteria) kutoka kwenye baadhi ya Masoko jijini Dar es salaam.
  • Hutumia mali ghafi kama vile Binder pamoja na mali ghafi zenye kiwango kikubwa cha Nitrogen
  • Pamoja na Brown material ambayo inatumika kuleta mchanganyiko wa uzalishaji wa mbolea.

Guavay sasa inapanga kuondoa kero kubwa ya takataka kwenye majiji yote nchini. Ikiwa kama fursa kwao katika kuongeza uzalishaji wa mbolea ya asili. Huku ikijiwekea malengo ya kuzalisha takribani tani 5000 kwa mwaka ikiwa ni pamoja nakutengeneza ajira zaidi.

Kampuni ya Guavay inaungana na Manispaa ya Kinonondoni katika kuitumia fursa hii ya pembejeo za kilimo. Mara baada ya manispaa hiyo kusaini Mkataba wa zaidi ya sh. bilioni 5.56 na kampuni ya ukandarasi  ya  CRJE ya nchini China. Mkataba huo ni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kiwanda  cha kuchakata taka kuwa mbolea aina ya mboji .

Hili kuweza kupata elimu na taarifa mbalimbali za uchambuzi wa kina endelea kutusikiliza kupitia DFM RADIO HAPA au pakua App yetu ya Dfm kwenye Google play store kutusikiliza live.

 

dfm.co.tz