Joshua Wenceslaus

Jukwaa la Biashara

Teknolojia imeonekana kuzungumziwa sana na wafanya biashara. Read More

Jinsi ya Kupata Mume Mwema

Ukisoma katika biblia  kitabu cha MWANZO 2:18 inasema Bwana Mungu akasema, si vyema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana nae. Read More

Kemea Pepo

Moja ya vitu ambavyo watu wengi wanaangalia kwenye nyimbo za injili ni maudhui ya wimbo huo. Kumekuwa na mijadala tofauti tofauti kuhusu nyimbo za injili na maudhui yake. Ukiacha maudhui hayo kuna mavazi pia ambayo huwa wainjilishaji ama waimbaji wa nyimbo za injili mengine yamekuwa maswali kwa watu, mengine yamekuwa majibu lakini mengine yamekuwa sintofahamu.

DFM katika kutafuta majibu hayo ilikutana na Emmanuel Mgaya ajulikanae kwa jina maarufu la Masanja Mkandamizaji. Masanja alitoa ushirikiano mzuri kujibu maswali aliyoulizwa na pia kueleza namna wimbo wake ulivyopokelewa na jamii. Wimbo wake unajulikana kwa jina la KEMEA PEPO na amesema yeye amefurahi kwa sababu wimbo wake umekuwa tiba.

Je, watamani kujua tiba hiyo ni ya aina gani? Sikiliza D-HITS mwenyewe usisubiri kusimuliwa uhondo huu wa kumsikia Masanja akitema cheche zake kuhusu tasnia hii ya muziki wa injili. Bofya hapa chini kwa kusikiliza.

Maisha baada ya Utajiri

Safari yoyote huwa na mwanzo wake lakini kuna wale ambao hawafiki mwisho, wengine wanabadili uelekeo na wengine humaliza vizuri safari. Kwenye maisha kuna kitu kinaitwa kujiongeza. Katika kujiongeza huko kuna kutumia njia za mkato au njia ya moja kwa moja ili kufanikisha kile ulichodhamiria. Alex William Kishimba ni mchungaji ambae alipitia katika maisha ya utajiri lakini baadae mambo yalibadilika.

Akiongea na DFM mchungaji Alex hakusita kufunguka na kueleza namna maisha yalivyokuwa matamu kwake na pale ambapo yalibadilika kwa ghafla na chanzo chake nini, katika pitapita yake alisema kuna sauti ambayo alikua anaisikia ikiongea nae kila mara. Sauti hiyo ilikua ikimnyima amani kabisa.

Kwa mwendelezo wa simulizi hii sikiliza kipindi cha D-TESTIFY ili kupata data kamili ya nini kilimkumba mchungaji huyo na ilikuaje. Baki hapa kwa uhondo huu.

Zitambue sifa za Mtumishi wa Mungu wa kweli

Ni Maisha uliyonayo yanakutakutambulisha kama nani mbele za waliokuzunguka?. Read More

Uchungaji na Uimbaji

Kushika mambo mawili sio tatizo japo inaweza kuwa changamoto kwa baadhi ya watu hasa pale ambapo yote yanaonekana kuwa na nguvu. Read More

Majaribu ni Mtaji

Majaribu yanapokuja yanakufanya ushindwe kusonga mbele au ndo yanakupa nguvu ya kusonga mbele? Read More

Mwarobaini wa dhambi za Ngono kwa vijana Wapatikana

Imekua ni jambo la kawaida hasa kwa vijana wa sasa kufanya ngono wakidhani ni kwenda na wakati na kufikia kuona wale wasiofanya hivyo ni washamba au wanamatatizo kibaiolojia. Read More

Utumishi wa Kanisa

Maisha uliyonayo yanakutakutambulisha kama nani mbele za waliokuzunguka. Wasifu huo unasadifu majina unayoitwa? Ni wazi kwamba utashtuka hasa kwa wewe ambae unaitwa majina kama vile mbabaishaji, tapeli au muongo. Majina unayoitwa hata kama ni kwa utani jaribu kuchunguza maisha yako na tabia ulizonazo. Kwa wale ambao wanaitwa watumishi wakati sio watumishi wajaribu kujichunguza pia.

Mtumishi wa Mungu Nyambele Zephania ambae amekulia maisha ya kanisani, anajaribu kueleza mfumo ambao ameishi na kupitia hayo basi utapata kujua mengi.

Unakumbuka wale waliokua wakiitwa maprofesa wakati wanasoma shule za secondary? Wale waliokuwa wakiitwa maripota, walimu, wachungaji na wasanii? Je, wewe ulikua unaitwa jina gani? Kuna athari zozote za kukubaliana na majina Fulani ambayo sio halisi? Fuatilia kipindi hiki cha D-IBADA hapahapa.

Ukongwe ni Uhodari

Ladha ya vitu kongwe je, huwa inakuwa na thamani ileile ukisikiliza wakati ukiwa umeshapita? Labda nikukumbushe ule msemo wenzetu wanasema “old is gold”. Sio mbaya mara moja moja kusikiliza vitu kongwe hasa katika tasnia ya uimbaji ni kitu ambacho kinakukumbusha wapi tumetoka. Kanisa la TAG Mwenge waliongea na DFM kutupasha habari kuwa kwaya yao imetimiza miaka 40 sasa.

Hivi unakumbuka vifaa vya muziki vilivyokuwa vinatumika zamani kutoa ala mbalimbali katika kuweka vionjo vya muziki? Mpangilio wa sauti ambao unasikika ukilinganisha na huu wa sasa unaona kuna tofauti gani iliyopo. Umuhimu wa kubadiisha style ama mitindo ya uimbaji upo wapi?

D-HITS ilipata kuzungumza na Imani Kwaya ambayo imetimiza miaka 40 na kuweza kutoa historia yao wapi walianza mpaka hapo walipo. Kwa kujifunza zaidi sikiliza (hapa)

dfm.co.tz